ARSENAL WALAZIMISHWA SARE YA 2-2 NA SOUTHAMPTON …




Yellow peril: Arsenal midfielder Santi Cazorla, centre, celebrates scoring his side's second against Southampton
ARSENAL imetia doa mwenendo wake wa Ligi Kuu ya England baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Southampton.
Matokeo hayo yanauweka rehani uongozi wa Arsenal kileleni mwa Ligi Kuu na iwapo Chelsea na Manchester City zitashinda michezo yao ya Jumatano usiku, washika bunduki hao watasogezwa hadi nafasi ya tatu.
Southampton waliokuwa wenyeji, walitangulia kupata bao katika dakika ya 21 kupitia kwa Fonte, bao lililodumu hadi mapumziko.
Arsenal wakasawazisha dakika ya 48 mfungaji akiwa ni Giroud.
French connection: Arsenal striker Olivier Giroud celebrates scoring the equaliser against Southampton
Dakika sita baadae Arsenal wakazidi kuchanua baada ya Cazorla kufunga goli la pili.
Hata hivyo sherehe za Arsenal hazikudumu kwani iliwachukua Southampton dakika mbili tu kusawazisha kupitia kwa Lalana.
Opening strike: Southampton's Jose Fonte, left, scores the first goal of the match against Arsenal at St Mary's
Arsenal wakapata pigo dakika ya 80 baada ya kiungo wao Flamini kufanya rafu ya kijinga na kulambwa kadi nyekundu.
Marching orders: Arsenal's Mathieu Flamini, in yellow, is given a red card by referee Lee Mason
Flamini sasa atakosa michezo mitatu: February 2: Crystal Palace (nyumbani), February 8: Liverpool (ugenini), February 12: Manchester United (nyumbani).
Southampton: Boruc 5, Chambers 6, Fonte 7, Yoshida 5, Shaw 7, Cork 5, Schneiderlin 5, S. Davis 5 (Do Prado 90), Lallana 7, Rodriguez 6, Gallagher 6 (Ward-Prowse 70, 6).
Arsenal: Szczesny 5, Sagna 6, Mertesacker 5, Koscielny 5, Monreal 4, Arteta 5, Flamini 3, Ozil 6, Cazorla 7 (Gibbs 86), Gnabry 5 (Oxlade-Chamberlain 70, 7), Giroud 7 (Podolski 90.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top