UMRI MZURI KWA MWANAMKE KUPATA MTOTO .. KUZAA

Tamaa ya kutaka kufanikiwa maishani  imeenea duniani kote. Hali imebadilika sana, jinsia ya kike inataka kujitosheleza kwa kila
kitu. Lakini mabadiliko ya kibaiolojia yanabaki vile vile mfano kuzeeka nk.
Mafanikio wanayowaza wengi ni utajiri wa pesa na elimu kubwa. Hii imesababisha wanawake wengi kusoma sana na kufanya kazi kupita kiasi, hata kupuuzia suala lakuzaa mapema.


Wengi wanashtuka ikiwa umri wao ni zaidi ya miaka 30, ndio wanakuwa na tamaa ya kuzaa. Kuchelewa kwao kuzaa kunaweza kuwa kwa taabu ama kuzaa watoto wenyematatizo mengi ya kiafya.
Kwa miaka mingi, wataalamu wengi wa afya ya uzazi bado wanaamini miaka 20-35 ndio umri sahihi kushika mimba na kuzaa.Pia, wengi wakifikiri matatizo mengi ya uzazi huongezeka baada ya miaka 35 na huwa zaidi baada ya miaka 40. Kwa wenzi wawili wanaoishi pamoja, kuchelewa kuzaa huathiri pia wenza wa kiume, ambapo mbegu za uzazi za mwanaume hudhorota kila mwaka upitaona watoto wamaotokana na wanaume wazee huwa na hatari zaidi ya kupata matatizo ya akili na matatizo ya chembe za urithi.



KUBALEHE
Kubalehe ni hatua muhimu sana lupotia ili kuweza kuzaa. Wastani wa kubalehe na kuvunja ungo kwa wasichana ni miaka 9-12 kwa sasa, ingawa miaka ya zamani ilikuwa kuanzia miaka 12-14. Baada ya kubalehe binti anakuwa na uwezo wa kushika mimba, japokuwa uwezekano huongezeka zaidi kati ya miaka 20-30, baada ya hapa uwezekano huanza kupungua.

Kulingana na The American College of Obstricians & Gynecologists uwezo wa wanawake kuzaa hupungua katika umri wa miaka 32 na hupungua kwa kasi zaidi katika umri wa miaka 37.

Uwezo wa wanawake kuzaa hupungua vile umri unaongezeka kwa kuwa wanawake wanapobalehe wanakuwa na idadi kamili ya mayai katika ovari zao. Namba hii hupungua vile mwanamke anavyozeeka. Pia mayai hayazalishwi kiurahisi kwa wanawake wenye umri mkubwa ukilinganisha na mabinti wadogo.

Kulingana na National Institute for Health & Clinical Excellence (NICE) ya Umoja wa madola (UK), kwa wanawake wenye miaka 35, ni wanawake 94 kati ya 100 wanaweza kupata ujauzito wakifanya ngono kwa
ukawaida ndani ya miaka 38, ni wanawake 77 kati ya 100 wanaweza kushika ujauzito.Magonjwa ya njia za uzazi kama Endometriosis na Uterine fibroids yanawatokea zaidi wanawake wenye umri mkubwa ambayo husababisha mwanamke kutoshika mimba.

Wanawake wenye umri zaidi ya miaka 35 wanaoamua kushika ujauzito wanakabili hatari ya kupanda kwa shinikizo la damu. Kupanda kwa shinikizo la damu wakati wa ujauzito huathiri kondo la nyuma (Placenta)
ambalo hutoa lishe kwa kijusi (kitoto kilicho tumboni) hali ambayo huathiri moja kwa moja ukuaji wake.

Pia, hatari ya kupata kisukari kwa wanawake wanaoshika ujauzito wakiwa namiaka 35 na zaidi, huongezeka sana. Kisukari kipindi cha ujauzito huongeza hatari ya kutoka mimba (Miscarriage), kuzaa
mtoto mwenye kasoro au kuzaa mtoto mkubwa kupita kiasi.

TAFITI YA HIVI KARIBUNI

Jambo la kushtusha, ni matokeo ya utafiti uliofanyika Sweden, watafiti wanadai hatari ya matatizo ya uzazi huanza mapema tupale mwanamke anapofikisha miaka 30. Utafiti uliochapishwa kwenye jarida la magonjwa ya uzazi (Journal of Obstetrics & Gynacology) uliofanywa na watafiti kutoka Taasisi ya Karolinska ya nchini Sweden umegundua katika nchi tajiri duniani wanawake huzaa wakiwa na umri mkubwa kitu kinachopelekea kuongezeka kwa hatari ya kuzaa watoto njiti (Preterm birth), ukuaji hafifu wa vichanga na kuzaa watoto wafu (Stillbirth).

Ili kubainisha hatari kati ya makundi tofauti ya umri ya wanawake wanaozaa kwa mara ya kwanza, watafiti walitumia takwimu za vizazi toka hospitali za Sweden na Norway, zilizokusanya taarifa za karibu wanawake milioni moja, kati ya mwaka 1990 na 2010. Hatari ya kuzaa watoto njiti (Premature birth) na kuzaa watoto wafu huongezeka kuanzia miaka ya 30 ingawa toka zamani, miaka 35 ndio ilitambulika kuwa mwanzo wa hatari kwa wanawake kupata watoto, lakini utafiti huu mpya unataja mwanzo tu wa miaka 30 hatari ya kupata matatizo katika uzazi huanza. Kwa kulinganisha kati ya kundi la umri wa miaka 25-29 na 30-34, wanawake wa miaka 30-34 wenye mimba za kwanza walikuwa na hatari ya kuzaa watoto njiti kwenye wiki 22-31 za ujauzito au kuzaa watoto wafu.

Kikosi cha watafiti kiligundua pia sababu zingine zinazoweza kuleta matatizo ya uzazi mfano wa sababu hizo ni kama kuvuta sigara au kuwa mnene kuliko kawaida. Ulla Waldenstrom, profesa wa kitengo cha afya ya wanawake na watoto katika taasisi ya Karolinska alisema : 'Tumeshangazwa na kuongezeka kwa hatari za uzazi katika umri mdogo sana.' Prof. Waldenstrom aliendelea ; 'Wanawake wanaweza ona hatari ni ndogo ila kwa jamii kiujumla kuna idadi kubwa ya matatizo yasiyo ya lazima kwao wanawake wanaozaa baada tu ya miaka 30. Hivyo nashauri wanawake na wanaume wapewe taarifa mashuleni juu ya umuhimu wa umri katika uzazi.'

 Ushauri kwa wanawake wenye umri zaidi ya miaka 30 wanaotaraji kuzaa,
 'NI bora kuepuka uvutaji wa tumbaku/sigara na kuepuka unene, kama inawezekana.'

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top