WAZO LA LEO... NANI KAMA MAMA?

Alijitahidi kula vyakula bora, kulala kwenye chandarua, kula mbogamboga za majani, na matunda, alijizuia kufanya kazi ngumu ili wewe uzaliwe salama.

Ukakaa tumboni kwake miezi tisa, siku yake ilipofika, hakubana miguu, hakukataa kwenda hospitali, alilia kwa uchungu, alinyofoa hadi nywele za kichwa chake kwa uchungu, ili wewe mtoto uzaliwe, alibana pumzi ya uhai wake ili wew uzaliwe.

Haikutosha, alikulea kwa taabu na shida, alikuwa tayari kwa lolote kwa ajili yako, alikulea kwa upendo, ukasoma, mme wake ambaye ni baba yako alikukataa ukiwa mdogo, kwa shida na kujibana huku akifanya kazi usiku kucha akakukuza na ukakua, ukafikia umri wa kutambua baya na jema.

Leo hii eti unapigana na mama? unamdharau mama?

Unamaisha mazuri, unakazi nzuri, lakini unashindwa kumhudumia
mama?

Unaishi katika nyumba nzuri, ya kifahari, mama yako analala kwenye nyumba inayovuja?

Jua na mvua vyote vyake?

jaribu kuiheshimu na kuithamini thamani ya mama katika dunia
hii..

Hakuna kama mama na hatatokea,
mpende sana mama yako sasa!!

Na kama huna maelewano mazuri na mama yako, ni muda wa kujirekebisha na kujirudi kwake ukiomba msamaha na kuumia kwa kitendo hicho !

Comment Hakuna kama mama yangu!!!!

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top