Zaidi ya abiria 10 wanusurika kupoteza maisha mkoani Iringa..... soma zaidi hapa

Abiria wakitoka kwenye gari hiyo baada ya kupinduka.


Abiria wakisaidiwa na wasamaria wema kutoka kwenye gari hiyo.



Wananchi wakiendelea kuwasaidia abiria hao ili kuwahishwa hospitalini kwa matibabu.



Hapa abiria wengine wakijiokoa wenyewe kutoka kwenye gari hilo.









ZAIDI ya watu kumi, wamejeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Iringa, baada daladala waliyokuwa wakisafiria kutoka Frelimo kwenda Tumaini, mjini Iringa kuacha njia na kuanguka.

Ajali hiyo imetokea jana mchana  majira ya saa saba, baada ya gari hiyo kushindwa kupanda mlima, na badala yake kurudi nyuma kabla ya kutumbukia kwenye mto.

Mwitikio imewashuhudia wasamaria wema wakiokoa majeruhi waliokuwa wamepanda daladala hiyo yenye namba za usajili, T 106 ABP ambao wote wamekimbizwahospitali kwa ajili ya matibabu.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Iringa, Ramadhani Mungi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo kwamba taarifa zaidi itatolewa baada ya uchunguzi kukamilika.

TUNAOMBA MAONI YAKO HAPA CHINI KUHUSU TAARIFA HII!!! 






Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top