Mchawi anaswa akiwanga kanisani,Arusha.....Soma zaidi hapa

Mchawi huyo akiwa anaombewa.
Baadhi ya vitendea kazi vya mchawi huyo.
Kazi Ipooo.
Katika hali isiyo ya kawaida mtu huyu ajulikanaye kwa jina la Shabani Hamis amenaswa akifanya mambo ya kishikina "uchawi" katika  kanisa la Ufufuo na Uzima Arusha.

Matukio ya kunaswa wachawi yamekuwa mengi kanisani hapo kutokana na uweza wa Mungu unaojidhihirisha kupitia Mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo, Frank Andrew.

Pamoja, na kukutwa bila nguo mtu huyo aliyekuwa amebeba vifaa ambavyo kwa mujibu wa maelezo yake, huvitumia kuwanga na kupaa ni pamoja na tunguli na kikapo cha mkoba wa uchawi. Tukio hilo la aina yake limetokea Usiku wa saa sita, wakati mkesha wa maombi ukiendelea kanisani hapo.
Baada ya maombi makali ya kuharibu uchawi katika anga la Arusha, ikafuatiwa na tukio hilo. Mungu ni mkuuu maana hapana uchawi wala Uganga juu ya watu wa Mungu.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top