Auawa kwa tuhuma za wizi wa baiskeli

Mtu mmoja aliyefahamika kwa majina ya Lughano John aliye na miaka 36 mkazi wa Ipinda Juu ameuawa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na wananchi wenye hasira kali walioamua kujichukulia sheria mkononi baada ya marehemu kutuhumiwa kuwa ameiba baiskeli.
Tukio hilo limetokea jana asubuhi ya saa nne katika kitongoji cha Lutusyo, kijijini Talatala katika Tarafa ya Ntebela wilayani Kyela mkoani hapa Mbeya.

Taarifa kutoka kwa mashuhuda wa tukio zinaeleza kwamba marehemu Lughano John alikamatwa na wananchi hao akiwa na baiskeli ya wizi na kisha kuanza kumshambulia kwa kumpiga hali iliyopelekea kifo chake.Wakati msako wa kuwatafuta watu waliohusika na tukio hilo ukiendelea, Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi amethibitishia kutokea kwa tikio hilo na  kutoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na badala yake wawe na tabia ya kuwapeleka watuhumiwa wanaokwamatwa katika mamlaka husika.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top