Ajilipua kwa mafuta ya taa jijini Dar

Kijana Nicholas Mhagama (25) aliyejilipuwa na mafuta ya taa akidai kunyanyaswa.AJILIPUA KWA MAFUTA YA TAA
Kijana mmoja Nicholas Mhagama (25), mkazi wa Makongo Juu Dar, juzi kati alijilipua na mafuta ya taa kisa kikidaiwa kunyanyaswa na babu yake. Tukio hilo lilitokea eneo la Makongo Juu Makaburini usiku ambapo kijana huyo na babu yake aliyemtaja kwa jina moja la Mhagama waligombana.Baada ya kijana huyo kuona isiwe tabu alijilipua na mafuta ya taa alipoona maumivu yanazidi akaanza kupiga kelele za kuomba msaada ambapo aliokolewa na kupelekwa Hospitali ya Mwananyamala na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya hali yake kuwa mbaya.
Waandishi walikwenda kufanya mahojiano naye hospitalini hapo ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Ndugu zangu naomba mnisaidie nipone kwani uamuzi niliouchukua haukuwa sahihi ni hasira za kilevi nilichokuwa nimekunywa.
“Yote haya ni sababu ya manyanyaso niliyopata kutoka kwa babu yangu ambaye alinifukuza nyumbani na kunitaka nikapange nyumba wakati nilikuwa na matatizo ambayo alikuwa akiyajua,” alisema Mhagama.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top