Chama cha mapinduzi CCM kimesema hakita sita kuwachukulia hatua viongozi watakao bainika katika sakata la tegeta Escrow.

Chama cha Mapinduzi  kimetoa tamko juu ya sakata la fedha za akaunti ya Tegeta Escrow na kusema hakitasita kuwachukulia hatua watumishi au viongozi wa Serikali,waliopewa dhamana ya  kuwatumikia wananchi  endapo watabainika kukiuka maadili na miiko ya uongozi wa umma.
Akitangaza  uamuzi  na msimamo huo kwenye mkutano wa hadhara Mkoani Lindi,Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM taifa ,Bwana Nape Nnauye, amesema kwa muda wote chama hicho kimekuwa kikiwashughulikia hata kuwavua nyadhifa  viongozi wote waliotuhumiwa kwa kukiuka maadili na miiko ya uongozi.

Akihutubia mamia ya wananchi wa Mkoa wa Lindi kwenye hitimisho la ziara ya siku nane mkoani humo, Katibu Mkuu wa chama hicho Bwana Abdurahman Kinana amewataka viongozi wa chama hicho kujitathimini kama wanakubalika kuliko kusubir i kuwajibishwa au  kutimuliwa kwenye uongozi.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top