Je unajua nini cha kufanya mumeo anapozaa nje ya ndoa?

Nianze kwa kumshukuru Mungu ambaye ameniweka hai mpaka siku hii ya leo, tunapokutana tena kwenye uwanja wetu huu kujuzana, kujadiliana, kuelimishana na kuzungumzia ishu mbalimbali zinazohusu uhusiano wa kimapenzi.

Leo nataka kuzungumza na wewe mama, dada, shangazi au mwanamke ambaye upo kwenye uhusiano wa kudumu, nikimaanisha umeolewa. Je, umewahi kugundua, kuhisi au kuambiwa kwamba mumeo mliyeishi pamoja kwa kipindi kirefu, amezaa mtoto na mwanamke wa nje?
Bila shaka kila mmoja atakuwa na majibu yake lakini katika mada hii nataka kuzungumza zaidi na wahusika, wanawake ambao wamewahi kutokewa na tatizo hili. Ni ukweli usiofichika kwamba wanaume wengi siku hizi wamekuwa na mchezo wa kuzaa nje ya ndoa.

Yaani amekuoa na mnaishi pamoja kama mume na mke, mmejaliwa kupata mtoto au watoto lakini kumbe nyuma ya pazia, yupo mwanamke mwenzako ambaye naye amezalishwa na mumeo. Je, unapaswa kufanya nini katika mazingira kama haya?

Mada ni nzito na ndiyo maana napenda zaidi kusikia kutoka kwa waliotokewa na tatizo hili kwani naamini kupitia wao, wengine watajifunza na hata watakapokuja kutokewa na hali kama hii, watajua namna ya kupambana nalo.

Je, ukigundua mumeo ana mtoto nje ya ndoa, utadai talaka, utamtafuta mwizi wako mpaka umpate na kumshikisha adabu, utamsaka mtoto ili umdhuru au utafanya nini? Hebu sikiliza ushuhuda wa mwanamke huyu ambaye nimewahi kukutana naye, akanisimulia mkasa wake ambao leo ndiyo ulionisukuma kuja na mada hii.

“Mimi ni mwanamke ambaye nimeolewa miaka minne iliyopita na kufanikiwa kupata watoto wawili. Wa kwanza ana miaka mitatu na huyu mwingine bado hajafikisha hata mwaka mmoja. Mume wangu ni mfanyakazi wa kampuni moja kubwa jijini Dar es Salaam.

Kwa kipindi chote tangu tuoane, tumekuwa tukiishi kwa amani na upendo wa hali ya juu mpaka miezi michache iliyopita ambapo nimegundua jambo baya mno katika ndoa yangu.“Nimegundua kwamba mume wangu ana mtoto mwingine ambaye ana umri wa miaka miwili.

Huyo mwanamke aliyezaa naye, mwanzo walikuwa wakifanya kazi pamoja ingawa sasa nasikia hayupo tena kazini kwa mume wangu ila nimesikia tetesi kwamba mume wangu ndiye aliyempangia chumba na anamhudumia kila kitu na siku nyingine huwa anaenda nyumbani kwake.

Nipo njia pandaa najihisi nakaribia kupatwa na ugonjwa wa moyo, ndoa yangu naiona chungu, namchukia sana mume wangu japokuwa ameniomba msamaha, sidhani kama nitamsamehe, naomba ushauri, nifanyeje?”

Hayo ndiyo maelezo aliyonipa mwanamke huyo ambaye kiumri bado ni mbichi na ndoa yake ndiyo hiyo ina miaka minne. Mpendwa msomaji wangu, bila shaka umeyaelewa vizuri maelezo ya dada huyu na tayari unayo majibu ya kumpa. Je, utamshauri nini?

KOSA LA MSINGI
Kosa la msingi ambalo mume wa dada huyu alilifanya ni usaliti. Yaani licha ya mwenzake kumpenda kwa moyo wote, aliamua kuchepuka na kwenda kwa mwanamke mwingine na kumpa ujauzito, kosa juu ya kosa.

Kosa la usaliti pekee ni baya na kama tulivyowahi kuzungumza kipindi cha nyuma, humchukua muda mrefu sana mtendewa wa usaliti kurudi kwenye hali yake ya kawaida na kurejesha mapenzi kwa aliyemtenda. Wengine hujikuta wakishindwa kabisa kusamehe na kusahau yaliyotokea.

Inapotokea usaliti umesababisha mtoto wa nje, uzito wa kosa huwa mkubwa zaidi na hata namna ya kulishughulikia, ni lazima wanandoa wote wawe makini sana kwani vinginevyo, huo unaweza kuwa mwisho wa ndoa au mapenzi kati ya wawili hao.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top