Serikali imewapeleka wakaguzi wa magari kufanya doria barabara kuu ilikupunguza ajali za barabarani

Serikali kupitia jeshi la polisi na mamlaka nyingine zilizopo kisheria imepeleka wakaguzi wa magari wanaofanya doria katika barabara kuu ili kubaini vitendo vyote vinavyokiuka sheria za uusalama barabarani.

Akijibu swali la mbunge wa Dole Mhe. Sylvester Mabumba Aliyeuliza ni hatua gani zinachukuliwa ili kukomesha kabisa ajali,na serikali inampango gani wakuwahudumia waliopatwa na ulemavu wa kudumu na ni watu wangapi wamepoteza maisha katika wimbi za ajali zilizotokea hivi karibuni.
Akijibu kwa niaba ya waziri wa  mambo ya ndani,waziri wa ncho ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma Mhe.Celina Kombani amesema jeshi la polisi limeendaa utaratibu wa lazima kwa kukagua magari  yote ya serikali na watu binafsi pamoja na kutoa elimu kwa njia ya redio na luninga,magezti na vipeperushi kuelimisha watumiaji wote wa barabara.

Aidha amesema takwimu zinaonyesha kuwa kuanzia januari hadi Desemba 2013 ajali za barabarani zilizkuwa elfu kumi na saba na mia saba ambapo januari hadi septemba 2014 ajali zilikuwa elfu kumi na moja na mia tato na kusisitiza serikali inaongeza juhudi ili kupunguza ajali hizo.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top