Waooo!....Walisema haolewi sasa kaolewa...Soma zaidi hapa


 
Walisema haolewi, sasa kakaolewa, Pongezi za Dhati zifike kwake SOLANGE KNOWLES ambaye ni Mdogo wake Beyonce, kwa kuweza kuingia katika Mchakato wa Kuwa kitu Kimoja na Mchumba wake ambaye This Time ni Mumewe, ALAN FERGUSON

SOLANGE alitamka Neno “Ndiyo” katika Mitaa ya NEW ORLEANS Nchini Marekani Siku ya Jana, JUMAPILI, ambapo Ilithibitika na Kuidhinishwa Kuwa tayari wawili hao ni Mwili Moja, Ila sina uhakika kama Moyo ni mmoja.

TTM iliweza kuzama kupitia Kitengo Chimbua Chimbua, na kupata Uhakika kuwa, Ndoa Hiyo ilikuwa ni Ya Kipekee na Tofauti sana, ambapo wawili hao walionekana kujawa na Nyuso za Furaha, huku wageni waalikwa wakiwa ni wachache lakini Muhimu sana

   Wageni Muhimu :
Kulikuwa na wageni Muhimu ambao walikuwa ni tazamio kubwa sana kuweza kuhudhuria Ndoa Hiyo ambayo ilioneakana kumvutia. Familia ya CARTER, nam,zungumzia JAY Z (Shemeji ake Solange), Beyonce (Dada ake Solange) pamoja na Mtoto wao Blue Ivy
 Tofauti na Hilo, mama Mzazi wa Solange pamoja na Beyonce, naye alitia Timu katika “Ubwabwa” huo ambao ulinukia balaa

     Mavazi Kwa Shughuli Nzima
Shughuli Nzima iling’aa sana ukizingatia Dressing Code ya Ndoa na Hafla yote Kiujumla, ilikuwa ni Mavazi yenye rangi Nyeupe. Jay Z alinyonga SUTI ambayo hakika itabaki kuwa gumzo na Kumfanya aonekane tofauti kabisa hasa kimuonekano.
 Maharus wote waligonga Kitu White, na kuifanya Ndoa hiyo kujawa na Weupe wenye Full happinesses

     Usafiri Ulikuwa Balaa
Tofauti na Vile ambavyo Tumezoea Siku zote, tunaonaga Maharusi wakiwa wamejificha ndani ya magari yenye Thamani sana na hata yakiwa Tinted, huku wengine wakiwa Kunako magari ya wazi ili tuone walivyopendeza, lakini huku imekuwa ni Toooofauti.
 SOLANGE na Mumewe ALAN FERGUSON, walipanda katika baiskeli ambazo pia zilipigwa Rangi Nyeupe

Kitu cha kushtua Kidogo, ni kwamba Mume alikuwa katika baiskeli iliyoonekana kuwa na Pancha, huku tukijiuliza kuwa what was That.
Pia baiskeli ya mamito SOLANGE, ilionekana kuwa na maua Fulani hivi ambayo yanaashiria huyu ndiye Mwali ati…

  Tujikumbushe
Hii itakuwa ni Mara ya Pili kwa Solange kufunga Ndoa, ambapo awali alifunga ndoa na jombaa anayefahamika kwa jina la DANIEL SMITH, na Walifanikiwa kupata mtoto DANIEL JULEZ ambaye hivi sasa ana Umri wa Miaka 10.









Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top