Fahamu tabia ya rafiki yako wa kike/kiume kabla ya kuingia katika Mahusiano...

Fanya uchunguzi wa kutosha kuhusu tabia, muono na imani ya rafiki yako hata kama hamuishi pamoja.
Zifuatazo ni njia ambazo unaweza kuzitumia kumchunguza rafiki yako kwa kina kabla ya kujiingiza nae kwenye mahusianao

>>Unaweza kumuuliza maswali kuhusu mahali anapoishi na familia yake kwa ujumla.
>>Jaribu kufanya mawasiliano ya karibu zaidi ili uweze kumdadisi,yeye aweze na uwezo wa kujieleza mwenyewe kwa undani zaidi.


>>kutumia watu wengine walio karibu naye.
Unapomchunguza mtu ambaye unafikiri anaweza kuwa mchumba wako inakubidi uwe na vigezo ulivyojiwekea ambavyo ungependa awe navyo.
Uchunguzi wa namna hiyo unaweza kukusaidia kujua tabia ya rafiki yako. Hata hivyo kufanya uchunguzi hakuna maana kwamba huhitaji kuwa naye kabisa. Bado unahitaji muda zaidi wa kuwa naye ili kumjua na kujenga uhusiano.

Jambo la kukumbuka ni kwamba tabia, siyo rahisi kufahamika na kuelezeka waziwazi, na hasa kama watu wako kwenye mapenzi. Mara nyingi katika mazingira haya siyo rahisi kuona kasoro. Vilevile tabia ya mtu huenda ikabadilika kulingana na umri na wakati hivyo ni vzuri ukawa makini katika uchunguzi wako na kuangali je rafiki yako ni mtu wa kubadilika badilika ili usije ukapata majibu yasiyokuwa sahihi.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top