UNIC yazindua ripoti ya Dawa za Kulevya Duniani

Uongozi wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataaifa (UNIC) umezindua ripoti ya Kupambana na dawa za kulevyaa ya Umoja wa Mataaifa, Uzinduzi uliofanywa Machi 4, Jijini Dar es Salaam.
Wakizungumza mbele ya waandishi wa habari, Afisa Habari wa Kituo Cha Habari wa Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo alibainisha ripoti hiyo imeweza kuchambua mambo mbalimbali dhidi ya dawa za kulevya na mikakati iliyofikiwa.

Ambapo alisema kuwa miongoni mwa mambo yaliyomo kwenye ripoti hiyo ni pamoja na kupungua kwa wimbi la kuingia kwa dawa za kulevyaa nchini hasa kupitia njia za bahari ya Hindi huku mji wa Mexico wa America, ukipunguza kwa asilimia kubwa matumizi ya dawa za kulevya.
Vuzo alibainisha kuwa, pia mikakati iliyofikiwa ambayo pia imo kwenye ripoti hiyo ni pamoja na mfumo wa kuwasaidia watumiaji wa dawa za kulevya wanaoacha kwa kuwapatia dawa maalum za kupunguza taratibu matumizi hayo.

‘Mipango ya kuwapatia wale wanaocha dawa maalum za kusaidia utumiaji wa madawa na pia dhidi ya kupambana na dawa maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi wa watumiaji” alisema Vuzo.
Aidha, alibainisha kuwa, Afrika Kusini katika bara la Afrika ndio inayoongoza kwa kuwa na njia nyingi za usafirishaji wa dawa za kulevya aina ya Cocaine na Heroine .

Kwa upande wake Mchambuzi Mkuu wa Mifumo ya Kompyuta wa Tume ya kudhibiti Ukimwi DCC, January Ntisi ,amesema wanashirikiana katika kupambana na dawa za kulevya na umoja huo kwani Tanzania ni miongoni nchi ambazo pia zinakabiriwa na tatizo hilo.

Alisema mwaka jana walikamata dawa tani 2.3 ambazo zingeingia nchini kungekuwa na kundi kubwa ambao wanatumia dawa hizo.

Kwa upande wake, Immaculate Nyoni ambaye ni Project officer UNODC alibainisha juhudi mbalimbali zinafanywa katika kukabiliana na wimbi la dawa za kulevya duniani kote ambapo kwa sasa angalau matumizi hayo yakiendelea kupungua.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top