Wema Sepetu,Miguu yangu haiwahusu hata kama ni mibaya.....



Staa  wa Bongo Movies, Wema Sepetu amewatolea uvivu baadhi ya watu ambao wameibuka kwa wingi mtandaoni wakiitoa karoso miguu ya staa huyo mara baada ya Wema kuweka picha kadhaa akiwa amevaa sketi ambayo inaonyesha miguu yake.

“Naomba niwaulize nyinyi mnaojiona miungu watu.... Mlitaka nijiongeze nyama miguuni kwangu au...?

"Ndo ilivyo na kuacha kuvaa nguo za kuionesha siwezi... Ntavaa tu... Yaani wala siwezi acha... Iwe mibaya iwe ina makovu iwe na michirizi ni ya Wema Sepetu... na kwakuwa ni yangu basi nita i embrace..

"Tuko pamoja eeh... Sasa muache vifimbo vyangu... maana ndo Mungu alonibarikia navyo…” Wema ameandika kupitia ukurasa wake mtandaoni

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top