Faiza Ally afunguka na haya kuhusu Mavazi, Mtoto, Dini na umaarufu aliokuwa nao...

Staa wa Bongo Movies, Faiza Ally  amefunguka mengi kuhusu yeye mwenyewe kwenye kipindi cha Nirvana kinachorushwa na EATV usiku wa jana.

Ishu kubwa ilikuwa kuhusu mavazi yake “Napenda kuvaa vitu ninavyovaa, sina mavazi special naweza kuvaa vyovyote, niliipenda idea ya kuvaa nepi (diapers) na sina tatizo nayo kabisa”

Faiza ni mama wa mtoto mmoja wa kike, kwenye upande wa malezi ikoje? “Mimi ni mama mzuri sana, ninamtazama mtoto wangu saa 24… mavazi yangu hayaingiliani kabisa na malezi ya mtoto wangu… namlea kwa mazingira ya heshima, heshima na nguo ni vitu tofauti… ninavaa mavazi ninayopenda na bado nina heshima kwa watu. Sio lazima kila mtu akubali ninachofanya, ninapofanya kitu kwa watu kukubali au kukataa ni matatizo yao”   Faiza Ally alieleza.



Kuna kitu chochote anachojutia kutokana na mavazi yake?  “Sina ninachojuta, niko sawa… tukio ambalo sijafurahia ni moja la kupelekwa Mahakamani na kunyang’anywa mtoto wangu kitu ambacho ninakifanyia kazi  na kinaenda vizuri.. sioni tukio  baya zaidi ya watu kunitukana na ni kawaida… ninaenjoy na ninapenda mavazi yangu” Faiza Alieleza.

Haya ndio maneno yake kuhusu nguo aliyoivaa kwenye KTMA 2015  “Idea ilikuwa ni nzuri mpaka pale ambapo nguo iliachana… lengo lilikuwa sio kuacha makalio wazi, ile nguo baada ya kukaa kwenye gari ilishuka na sehemu ya makalio ikabaki wazi… Wakati natoka nyumbani ilikuwa imekaa tu vizuri, nilivyoshuka kwenye gari sikujiangalia, nilipofika red carpet nikapigwa picha”

Anatoka kwenye familia inayofuata Dini?  “Baba yangu sijawahi kumwona anakwenda Msikitini, sio kwamba naikana dini lakini sijazaliwa kwenye familia ya kidini.. maisha yangu yako hivi miaka yote na hakuna kilichobadilika kwenye maisha yangu… nafurahia maisha yangu”

Huu ndio ushauri wake kwa wasichana kuhusu ishu ya fashion za mavazi  “Wasichana wajue kwamba kilicholeta gumzo ilikuwa bahati mbaya, ila wawe huru wavae vitu wanavyovifurahia ila isitokee kama ile… kuna mavazi navaa na kuna mavazi siwezi kuvaa”

Matukio ya mavazi yake yamempa umaarufu? Amepanga kufanya chochote? “Sijapanga chochote, sikujua kama itakuwa ni umaarufu… mimi ni mwigizaji na ninaandika kitabu, labda kwa kazi zangu hizo… kipande kilichoonekana sio maisha yangu yote, ni sehemu ya mwili… Faiza ni mwanamke mzuri, anayejielewa, mwenye akili timamu, mama bora, anayejipenda, mtu wa watu”   Faiza Ally.

Kwenye Interview hiyo alikuwepo pia mwanamitindo Ally Rehmtullah, haya  ndio maneno yake kuhusu nguo ya Faiza “Ubunifu wake ulikuwa mzuri labda mawasiliano kati ya yeye na mbunifu wake hayakuwa mazuri, vazi kama lile kwa utamaduni wetu lazima watu watashtuka watakusema, ni muhimu kujua yeye mwenyewe Faiza alikuwa anataka nini… Naamini ilikuwa bahati mbaya, ingekuwa ni mimi ile gauni nisingevaa”  Ally Rehmtullah

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top