Baada ya kupigwa chini katika kinyang’anyiro cha kuwania Ubunge wa viti maalum kwa tiketi ya CCM Morogoro Vijijini, staa wa filamu Bongo, Wastara Juma ametoa kituko cha mwaka baada ya kusema amejisikia vizuri kwa madai kuwa atapata muda wa kujipanga zaidi.
Akipiga stori na gazeti hili, Wastara ambaye alishika nafasi ya pili katika kinyang’anyiro hicho, alisema amefurahi kwa nafasi hiyo kwani amethubutu na hakuitegemea, hivyo anajipanga kuwa karibu na walengwa wake ambao ni walemavu ili kujua matatizo na malalamiko yao.

“Ukweli nimejitahidi sana maana nimeshindana na mtu aliyekaa madarakani kwa miaka 20 na ni mara yangu ya kwanza kugombea ubunge, nimethubutu, nimepata kura 254 siyo mchezo japo anayetakiwa ni mmoja lakini jina langu litaenda kujadiliwa na nitafikiriwa,” alisema Wastara ambaye alibwagwa na Magreth Mkanga.
Post a Comment