Watuumiwa wa Ujambazi 27 wenye silaha wakamatwa mkoani pwani



Jeshi la polisi Mkoa wa Pwani  limefanya msako mkali katika mapori mbali mbali  na  kufanikiwa kuwakamata   watuhumiwa  wa ujambazi  27 pamoja na   risasi 153,bunduki 2  mabomu 3  ambavyo  walikuwa wakivitumia katika matukio ya uharifu.

Kwa mujibu wa  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishina mwandamizi Jafari Ibrahimu amesema kwamba watuhumiwa hao wamekamatwa baada ya kufanyika operesheni katika magenge yaliyopo vichakani na kuwakuta watuhumiwa hao wakiwa wamejificha pamoja na silaha walizokuwa wanazitumia kufanyia uhalifu

Ameongeza kuwa  wameamua kufanya  operesheni  hiyo  kutokana na kuongezeka kwa uharifu katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani na kuwakamata watuhumiwa hao  ambao wengine walikutwa na vifaa mbali mbali ikiwemo visu mapanga,pamoja na nyaya tatu za milipuko ya mabomu.

Katika zoezi hilo pia waliweza  kukamata madawa ya kulevya aina aya bangi gunia 18 na mirungi kilo 124,lita 88 za pombe ya moshi pamoja na mitambo yake mitatu ya kutengenezea noti bandia 370 na meno ya tembo.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top