Kufuatia kupigwa mwereka kwenye Ubunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Singida, staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amekiri kwamba kilichomponza katika kinyang’anyiro hicho ni skendo za ngono hivyo kwa sasa atakuwa makini ili asichafuke.
Akizungumza na gazeti hili baada ya kupokelewa kishujaa na kuacha historia jijini Dar aliporejea kutoka Singida wikiendi iliyopita, Wema alisema mashabiki wake hawatamsikia tena na skendo hizo huku akiahidi kuibuka na bonge la ‘surprise’.

“Shukurani zangu zipo palepale kwa mashabiki wote wanaonisapoti.
“Ninachowaahidi kwa sasa ni kuwa makini na skendo lakini pia kuna kitu cha kushtua nitafanya hivi karibuni ambacho kitaibua surprise (mshtuko) nzito kwa mashabiki wangu,” alisema Wema.
Katika mapokezi hayo ambayo gazeti hili lilikuwa mstari wa mbele, makundi ya mashabiki wake na yale ya Team Wema yalipeana taarifa kupitia mitandao ya kijamii kuwa kipenzi chao, Wema angefika Dar, Jumapili iliyopita ambapo taarifa zilisema kuwa walikutana kimyakimya na kuandaa mapokezi ya Madam.
Mishale ya saa 7:00 mchana ndipo Team Wema na mashabiki wake wengine walianza kumiminika maeneo ya Kimara-Baruti jijini Dar wakiwa na mabasi ya kukodisha, pikipiki na magari binafsi ambapo shamrashamra za kila aina zilifanyika.
Pia kulikuwa na ngoma ya Kibao-Kata, michezo ya pikipiki huku nyimbo za kumsifu Wema zikiimbwa.
Kama hiyo haitoshi, amshaamsha hiyo ilikuwa ikifanywa kila sehemu ambapo mastaa walikuwa wakitokea maeneo hayo kwa ajili ya kumsapoti Wema.
Umati uliojitokeza walianza kulipuka kwa shangwe baada ya kumuona Meneja wa Wema, Martin Kadinda aliyeingia katika eneo hilo akifuatiwa na Petit Man ambaye alifuatana na wasanii wa Bongo Fleva, Mirror na Suma Mnazareti.
Mashabiki hao wa kila kada huku watoto wakifurika kumuona Wema walionekana kuwa na mapenzi ya hali ya juu huku mama mmoja mwenye ujauzito mkubwa akionekana akijichanganya kila kona bila kujali hali yake.
Wema aliingia katika maeneo hayo (Kimara-Baruti) akiwa ndani ya gari aina ya Toyota Land Cruiser ambapo alishuka na kuingia ndani ya BMW lililoletwa kumpokea ambapo alitokea kwenye paa na kuanza kusalimia mashabiki wake waliolipuka kwa furaha na wengine wakiangua kilio cha furaha.
Kuna wengine walishindwa kujizuia wakajikuta wakimfuata Wema wakimbusu na kumshika nywele zake kama vile siyo binadamu.
Wema alilazimika kugawa cheni na pete zake za dhahabu kwa mashabiki wake ili kuwatuliza huku akiwashukuru kwa kumpokea na kuwaaga kuwa anakwenda nyumbani kwake Kijitonyama ambapo msafara wake ulisababisha foleni ya zaidi ya robo saa njia nzima ambapo alikuwa akisindikizwa na pikipiki.
“Yaani Madam amepokelewa na watu kama rais vile, duh! Sijawahi kuona, amekosa ubunge lakini shamrashamra yake kama vile ameshinda!” Alisema mmoja wa mashabiki wa Wema aliyevalia fulana zenye nembo iliyoandikwa ‘Wema’.
Habari zilieleza kwamba, kinachoonekana Wema anajipanga upya ili kujiimarisha kisiasa kwa ajili ya baadaye hivyo atajitahidi kuwa mbali na skendo hasa za wanaume.

Post a Comment