Lowassa kuchukua Fomu ya Urais Jumatatu Saa tatu kamili asubuhi

Chama  cha  Demokrasia  na  Maendeleo (CHADEMA) kimetoa taarifa kuhusu utaratibu wa Mgombea wa UKAWA, Edward Lowassa kuchukua Fomu za  Urais  katika  ofisi  za  Tume  ya  Taifa ya  Uchaguzi.

Akitoa  taarifa  hizo  mbele  ya  waandishi  wa  habari  leo  mchana, Naibu Katibu  Mkuu  wa  Chadema, ndg  Salum  Mwalimu  ambaye  kwa  sasa  anakaimu  nafasi  ya  Katibu  Mkuu  wa  Chadema  amesema  Mh. Lowassa  atachukua  fomu  hizo  Jumatatu  ya  tarehe 10, Agosti  2015, saa  tatu  kamili  asubuhi.
Mwalimu  amesema  msafara  wa  Lowassa  utaanzia  katika  ofisi  za  CUF  zilizopo  Buguruni  ambapo  utaelekea  ofisi  za  Tume  ya  Uchaguzi  kwa  ajili  ya  Kuchukua  fomu.

Baada  ya  zoezi  la  kuchukua  fomu, msafara  huo  utaelekea  makao  makuu  ya  CHADEMA  Yaliyoko  Kinondoni  ambapo  kutakuwa  na  shamrashamra  kidogo.

Hapa  kuna  sentensi 14  ambazo  mwalimu  amezitamka  wakati  akiongea  na  waandishi  wa  habari.

1.Tupo ktk Kipindi cha Uchaguzi na Wagombea Urais wa Z'bar na TZ Bara tayari tumewatangaza'-

2.Tarehe 10 Mgombea Urais wa TZ ataongozana na Mgombea mwenza wake kwenda kuchukua Fomu NEC.

3.Mh. LOWASSA atasindikizwa na Viongozi Mbalimbali wakubwa wa Vyama vinavyounda Umoja wa UKAWA.

4.Zoezi la Uchukuaji wa Fomu msafara utaanzia Ofisi za CUF Buguruni kuelekea Tume ya Uchaguzi.

5.Msafara utaishia Ofisi za CHADEMA K'ndoni ambapo kutakuwa na shamrashamra kidogo.

6.Mh. LOWASSA atazunguka Mikoani kutafuta wadhamini, Watz wana hamu kumuona LOWASSA akiwa na combat ya CDM.

7.Mtaniwia radhi kwamba hatoweza kuzunguka nchi nzima, tutatangaza maeneo ambayo atapita.

8.Baada ya Uzinduzi wa Kampeni Dar, LOWASSA atapita Majimbo yote kama alivyoahidi.

9.LOWASSA Tarehe 13 atashiriki na Viongozi wengine kwenye Mazishi ya Mzee KISUMO Mkoa wa K'njaro.

10.Hatuwezi kuwazuia watu wanaotaka kumsindikiza LOWASSA kuchukua Fomu Ofisi za NEC.

11.Kazi ya kugawanya Majimbo ya Ubunge imekamilika, kazi imekamilika salama na kwa amani.

12.Kuna jambo linaendelea watu wanaambiwa wakusanye Kadi zao za Kupigia Kura.

13.Yoyote anayeambiwa atoe kadi au atoe namba ya Kadi yake ya Kupigia Kura akatae.

14.UKAWA haijayumba kwa namna yoyote kwa kuondoka kwa Prof. LIPUMBA, tunasonga mbele.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top