Mafuriko!! Dr. Magufuli apokelewa na maelfu ya watu mkoani Ruvuma

Mgombea urais kupitia chama cha mapinduzi Dr John Pombe Magufuli amepata mapokezi makubwa katika mkoa wa Ruvuma na kuahidi kuwa katika kipindi chake cha uongozi Tanzania itakuwa nchi inayotegemea uchumi wa viwanda na maliasili pamoja na kutoa fursa za uwekezaji wenye tija kwa taifa kwa wawekezaji wazalendo na wa kigeni.

Dr Magufuli ametoa ahadi hiyo na kuwataka watanzania kumuamini kwa kuwa anamaanisha kile anachokiahidi kwa kuwa anamuogopa mungu na kuongeza kuwa anatamani kuiona tanzania inayotegemea uchumi wa viwanda na maliasili badala ya kuwa na lundo la kodi kero kwa wananchi na kwamba atatoa fursa na upendeleo maalum kwa wawekzaji wazawa lakini pia wageni ili kuwa na uwekezaji wenye tija kwa taifa.


Akizungumza na umati wa wananchi waliojitokeza katika uwanja wa majimaji kusikiliza sera za Dr Magufuli aliyekuwa mbunge wa Songea mjini Dr Emmanuel Nchimbi amewataka watanzania kumchagua Dr Magufuli kwa kuwa ndie kiongozi pekee anayeahidi na kutekeleza.

Akitokea mkoani Njombe kuingia mkoani Ruvuma ambapo ametumia kivuko kuvuka mto ruhuhu ambapo wananchi wamelalamika kupoteza maisha kwa kuliwa na mamba wakati wa kuvuka mto huo lakini pia wananchi wa mbinga wakimtaka kutafuta masoko yenye uhakika kwa ajili ya mazao yao.

Akijibu kero hizo Dr Magufuli amesema endapo atachaguliwa kuwa rais wa awamu ya tano itakuwa ni marufuku kwa serikali yake kukopa mazao kwa wakulima na kwamb watalipwa papo kwa hapo lakini pia akaahidi kujenga daraja katika mto ruhuhu.

jumanne ya september mosi Dr Magufuli anatarajiwa kuendelea na ziara yake ya kujinadi kwa watanzania kupata fursa ya kuliongoza taifa la tanzaia mkoani mtwara.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top