Chama cha mapinduzi CCM kimesema kikifanikiwa kuingia madarakani katika kipindi kijacho kitahakikisha kinatekeleza ilani yake ya kutoa asilimia thelasini ya tenda za kazi za halmashauri kwa vikundi vya vijana vilitakavyo sajiliwa rasimi na asilimia kumi za mapato yake yatatengwa kusaidia vikundi hivyo ili kuwawezesha kujikwamua na ugumu wa maisha.
Mgombea mwenza wa rais kwa tiketi ya CCM Samia Suluhu Hasani ameyasema hayo katika majimbo ya Kibaha mjini vijijini na Kisarawe mkoani Pwani ambapo amesema kutokana na ajira kuwa ngumu kwa vijana CCM imeamua kuweka mpango huo ili kuwa kwamua kiuchumi nawo wanufaike na rasilimali zilizopo katika maeneo yao.

Viongozi wa CCM waliyo ongozana na mgombea mwenza wamesema kwa kawaida wapinzani wanachangia kuweka changamoto katika kusukuma ufanisi wa serikali lakini katika utawala CCM ndiyo chenye uwezo zaidi ya vingine hivyo kuna kila sababu ya kukipa kura.
Kwa upande wao wagombea wa ubunge katika majimbo ya Kibaha mjini vijijini na Kisarawe wamepata nafasi ya kunadi sera za chama chao kuahinisha changamoto pamoja na mafanikio na mambo watakayo yafanya endapo watafanikiwa kuingia madarakani.

Post a Comment