Kanisa katoliki sasa kuvunja ndoa

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis jana alieleza mabadiliko mapya yanayolenga kuwarahisishia Wakatoliki kuvunja ndoa zao na kuoa upya.

Dhamira hiyo ni ishara nyingine ya dhamira ya Papa huyo kutaka kulifanya Kanisa Katoliki liwe rafiki zaidi na kuendana matakwa ya walio wengi.

Akizungumza kuhusu mabadiliko hayo, Papa alisema si haki kwa wenzi kuishi muda mrefu ‘wakikandamizwa na wingu la shaka’ kuhusu uhalali wa ndoa zao.

Ikumbukwe kwamba ni msimamo wa Papa kumkatalia Mfalme Henry the VIII wa Uingereza kumtaliki mkewe Catherine wa Aragon katika karne ya 16 uliosababisha England ijitenge na Rome na kushuhudia kuundwa kwa Kanisa la England huku mfalme akiwa mlinzi wa Imani wa kanisa hilo.
Mabadiliko makuu matatu aliyotangaza  Papa jana ni   kuondoa mchakato wa mapitio ya mara ya pili wa uamuzi wa kutoa talaka kupitia mahakama ya kanisa kabla ya ndoa kuvunjwa.

Mengine ni kuwapatia maaskofu uwezo wa kuharakisha na kuvunja ndoa   wenzi wanapoamua wenyewe katika mazingira fulani kama vile ukatili katika ndoa au uasherati na mchakato huo wa talaka kuwa bure, isipokuwa kwa kulipa ada ndogo kwa ajili ya gharama za  utawala.

Kabla ya sheria hiyo, Wakatoliki waliotaka talaka walihitaji kibali kutoka kwa mahakama mbili za kanisa, wakati sheria mpya inabakiza moja ingawa rufaa bado zinaruhusiwa.

Kabla ya sheria hiyo, wanandoa wa Wakatoliki wanaotalikiana bila idhini ya kanisa na kuolewa upya walihesabiwa kama wazinifu na hawakuruhusiwa kupokea komunio.

Lakini kwa mujibu wa  utaratibu mpya, wanaotalikiana wakioa au kuolewa tena watabakia kuwa wafuasi wa kanisa hilo.

Mwaka jana Papa aliunda tume ya wanasheria wa kanisa hilo  kuboresha na kurekebisha taratibu hizo  kurahisisha wanandoa kuachana na kupunguza gharama.

Mageuzi hayo yalikuja katika mfumo wa nyaraka mbili zinazoitwa ‘motu proprio’, neno la kilatini lililobuniwa na Papa mwenyewe.

Taratibu hizo zitakuwa rasmi kama sehemu ya sheria za kanisa (canon law) ifikapo Desemba 8 mwaka huu wakati Papa atakapoanza kutangaza Mwaka wa Jubilee ambao kwa kawaida huhusishwa na msamaha.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top