Mahujaji wanne wa Tanzania wafariki Mecca

Watanzania wanne wamethibitishwa kufa katika tukio la kukanyagana jana huko Mina katika mji wa Mecca, ikiwa ni miongoni mwa mahujaji 717 waliopoteza maisha katika tukio hilo wakati wa siku ya mwisho ya Hija.

Taarifa ya Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abu Bakari Zuberi iliyotolewa akiwa Mecca imewataja watanzania watatu waliokwisha tambulika majina yao kuwa ni Bi. Mwanaisha Hassan Juma, Mkungwe Suleiman Hemedi na Sefu Saidi Kitimla.

Mtanzania mwingine mwanamke aliyekufa jina lake bado halijatambulika, pia yupo raia mmoja wa Kenya Bi. Fatuma Mohammed Jama ambaye alisafiri Mecca kwa kutumia wakala wa Tanzania.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top