Sumaye atakiwa kujibu tuhuma za Meno ya Tembo

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Hai kimemtaka Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye kujibu tuhuma zilizokuwa zikimkabili kuhusu gari alilokuwa akitumia kukutwa na meno ya tembo yenye thamani ya Sh milioni 100 mwaka jana.

Katika tukio hilo lililojiri Machi 26, 2014 pembe hizo zilikutwa zikiwa zimebebwa na gari lenye namba za usajili STK 8394 lililokuwa likitumiwa na Sumaye. Gari hilo lilikamatwa eneo la Ulanga mkoani Morogoro ambapo katika majibu yake (Sumaye) alidai ni mchezo mchafu uliofanywa na mafisadi kuzuia ndoto zake za kugombea urais.

Mwenyekiti wa CCM wilayani Hai, Amini Uronu alisema hayo jana mjini hapa wakati akijibu baadhi ya madai yaliyotolewa na Sumaye ambaye kwa sasa amejitoa ndani ya CCM na kuungana na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Katika madai ya Sumaye kwa wananchi katika viwanja vya Half London wilayani Hai, alitaka CCM iwaeleze Watanzania kuwa nani anafanya biashara ya pembe za ndovu.

Viongozi wa Ukawa juzi, walifanya mikutano wilayani Hai na kufanya upotoshaji wa masuala mbalimbali, moja ya mambo Sumaye alihoji juu ya biashara ya pembe za ndovu… Sasa sisi tunataka ajibu tuhuma baada ya gari lake kukutwa na pembe hizo, asiwahadae wananchi amtaje mmiliki wake,” alisema Uronu.

Uronu alidai pia katika madai yake kwa wakati huo, Sumaye alimtaja Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa ambaye sasa ni mgombea wa urais kupitia Chadema, kuwa ni miongoni mwa waliofanya njama hizo.

Pia Sumaye katika kauli zake alidai kuwa iwapo CCM ingemteua Lowassa kuwa mgombea urais kupitia chama hicho yeye angejitoa, leo anakuja kuwahadaa wananchi wakati sasa ndiyo anamnadi kuwa ni mtu mwadilifu na mchapakazi,” alisema.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top