Rais Magufuli Awakuna Waingereza

Balozi wa Uingereza nchini, Diana Melrose amewahakikishia wafanyabiashara wa Uingereza kwamba Tanzania ina mazingira mazuri ya uwekezaji na Serikali ipo tayari kushirikiana nao.

Melrose aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na ujumbe wa wafanyabiashara wakiongozwa na Chama cha Wafanyabiashara wa Uingereza (London Chamber of Commerce), Kitengo cha Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

Alisema amefanya mazungumzo na Rais John Magufuli hivi karibuni na kumuonyesha dhamira ya kuleta mabadiliko ili wananchi wapate huduma za jamii.

Makamu wa Rais wa London Chamber of Commerce, Subhash Thakrar alisema ili kukuza uchumi lazima kuwapo na kampuni nyingi zinazochipukia.

Mshauri wa kimataifa wa biashara kutoka Uingereza, David Billingsby alisema ziara hiyo itatoa fursa za mafanikio kwa biashara zitakazoshiriki.

Alitoa mfano kwa mshiriki ambaye mwaka jana alikuwa mtaji wa kuanzisha shule ya kimataifa.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top