Wanafunzi wa kike nchini wahimizwa kusoma masomo ya Sayansi na Hisabati.

Makamu wa rais Mh Samia Suluhu Hassan ameitaka taasisi ya wahandisi wanawake nchini kuandaa kampeni mbalimbali za kuwahimiza wanafunzi hasa wa kike kusoma masomo ya Sayansi na Hisabati pia wajitambue na kuithamini nafasi yao katika kuchangia maendeleo ya nchi kupitia fani ya Sayansi na Teknolojia.

Akifungua kongamano la wahandisi wanawake Mh Samia amesema licha ya kupata mafanikio ya kuongeza idadi ya wahandisi wataalamu wanawake kutoka 39 mwaka 2005 hadi 298 mwaka 2015 bado idadi hiyo ni ndogo ni moja ya changamoto ambazo kitengo cha wanawake wahandisi kinatakiwa kufanyia kazi ili kuhakikisha idadi hiyo inaongezeka mwaka hadi mwaka.

Akizungumza katika kongamano hilo msajili wa wahandisi Injiania Stephen Mlote amesema katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili wahandisi wanawake serikali ya Norwey imekuwa ikifadhili miradi mbalimbali kwa kutoa mafunzo kwa vitendo ambapo awali ilitoa sh bilioni 3 iliyoendeleza wanawake 291 na sasa imetoa bilioni 4.3 kutoa mafunzo yanayohusiana na mafuta na gesi.

Naye mwenyekiti wa kitengo cha wahandisi wanawake cha taasisi ya wahandisi Injinia Alice Isibika amemweleza makamu wa rais kuwa licha ya kukabiliwa na tatizo la uhaba wa rasilimali fedha changamoto nyingine ni namna ya kuwapata wanawake wahandisi ili kufanyakazi kwa ushirikiano.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top