>

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu Octoba 24




























Mpenzi Mpya wa Wema Sepetu Afungukia Penzi Lao

‘Model’ anayedaiwa kuchukua nafasi ya Idriss kwa kutoka kimapenzi na mrembo Wema Sepetu, amejikuta akiweka hadharani mahaba yake kwa mrembo huyo kwa kutoa maelezo yanayothibitisha kuwa hivi sasa yeye na Wema ni wapenzi.

Kijana huyo anayefahamika kwa jina la Calisah, alikumbana na kibano kizito kupitia kipindi cha FNL kinachuruka kila Ijumaa kupitia EATV, pale alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa mahusiano yake na mrembo huyo ambaye alikuwa Miss Tanzania mwaka 2006.

Calisah alisema Wema ni msichana mrembo na mwenye mvuto kwa kila mwanaume, hivyo hata yeye anavutiwa naye na anapenda kuwa naye katika mahusiano, lakini akagoma kusema iwapo tayari wameanza mahusiano au la.

Calisah pia alijifagilia kuwa uzuri wake ndiyo uliomfanya Wema kumzimikia na kuwatosa wote aliokuwa kuwa nao.


“Wema is a beautiful girl, sexy and every man’s dream, na mimi pia ni mvulana mzuri ambaye mwanamke yeyote angependa kuwa na mimi, akiwemo Wema mwenyewe, siwezi kusema moja kwa moja kwamba sisi ni wapenzi, lakini lakizima ujue kuwa Wema ni mzuri na mimi mzuri”

Alipotakiwa kutamka sababu za kumpora Wema kutoka kwa Idriss, Carissa amesema hamjui vizuri Idriss, na kwamba hakumbuki kama Tanzania imewahi kuwakilishwa na mtu anayeitwa Idriss katika mashindano ya Big Brother Afrika akisema “Who? Idriss, kwani amewahi kuwa Big Brother? Which year?”

eatv.tv

Joketi Kujenga Viwanja vya Michezo

Mrembo, Jokate Mwegelo ameahidi kujenga viwanja vya michezo kwa shule ya Sekondari ya Majani ya Chai iliyopo Vingunguti jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika mahafali ya nane ya shule hiyo, Jokate alisema atajenga viwanja hivyo kupitia kampeni yake yake ya kuchangia jamii ijulikanayo kwa jina la “Be Kidotified.”
Amesema ameguswa na changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo na kuamua kusaidia kwa kupitia kampeni yake hiyo.

Tayari Jokate amekabidhi viwanja katika shule ya Sekondari ya Wasichana wa Jangwani.

Mfalme Mohammed Vi wa Morocco Awasili Jijini Dar, Apokelewa na Mwenyeji Wake Rais Dkt Magufuli


Mwigizaji wa Bongo Movie JB Anusurika Kifo Katika Ajili ya Gari

Mwigizaji wa filamu na mtayarishaji, Jacob Stephen ‘JB’ Ijumaa hii amenusurika kifo katika ajali ya gari.

Mwigizaji huyo ambaye hivi karibuni alikuwa mkoani Arusha katika shindano la Mama Shujaa, amewataka mashabiki wake kutambua kwamba anaendelea vizuri pamoja na wanzake ambao walikuwa kwenye gari hilo.
Asanteni wote mlionipa pole kwa ajali ya jana,” aliandika JB instagram. “Hakika Mungu ni Mwema, nipo poa mimi na wenzangu wote. Namshukuru sana Mungu.Thank you JESUS,”

Kwa sasa mwigizaji huyo anafanya vizuri na filamu yake, ‘Kalambati Lobo’.

Ajali za barabarani nchini Tanzania zinatajwa kuwa ni moja kati ya matukio ambayo yanasababisha vifo vingi nchini.

Ndalichako, Mahiga Wawavuruga Chadema, CCM Wajichagulia Meya Bila Mpinzani

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) leo kimeususia uchaguzi wa Meya na Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, hali iliyopelekea wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufanya uchaguzi peke yao na kuwapigia kura wagombea wao bila upinzani.

CCM wamemchagua Benjamin Sitta kuwa Meya wa Manispaa hiyo kwa kura zote 18 za wajumbe wa chama hicho. George Manyama amepata Baraka za wajumbe hao wa chama tawala kuwa Naibu Meya wa Manispaa hiyo.
Chadema waliususia uchaguzi huo kwa madai kuwa CCM wamechakachua kwa kuwaleta Profesa Joyce Ndalichako (Waziri wa Elimu) na Balozi Agustine Mahiga (Waziri wa Mambo ya Nje) kupiga kura katika Manispaa hiyo ili hali waliapa na kusajiliwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala. Hivyo, sio wajumbe halali wa Kinondoni na hawakupaswa kupiga kura.
Balozi Augustine Mahiga

Wajumbe wa Chadema wanadai kuwa uchaguzi uliofanywa na CCM peke yao sio halali kwani pamoja na mambo mengine akidi ambayo ni 2/3 ya wajumbe waliopaswa kufanya uchaguzi huo kuwa halali haikutimia.

Chadema imepanga kupinga uchaguzi huo mahakamani

Watu 2 Wanashikiliwa na Polisi kwa Kukutwa na Meno ya Tembo Simiyu

Jeshi la Polisi mkoani Simiyu linawashikilia watu wawili kwa kukutwa na meno ya tembo yenye uzito wa kilo sita ikiwa ni pamoja na silaha moja, huku mtu mmoja akishikiliwa kwa tuhuma ya kumbaka mtoto wa chekechea mwenye umri wa miaka saba.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Kamishina Msadizi Mwandamizi Onesmo Lyanga amesema Oktoba 10 mwaka huu majira ya saa tatu usiku katika kijiji cha Bumela kata ya Bumela wilayani Itilima askari polisi wakishirikiana na askari wa wanyamapori kutoka Maswa Game Reserve wakiwa katika msako waliwakamata wawindaji haramu.
Waliokamatwa ni Sendama Musa na Busule  Nzugu wakiwa na pembe mbili za ndovu zenye uzito wa kilo 6 ikiwa ni pamoja na silaha moja yenye uwezo kufanya kazi kama silaha aina ya short gun na kisha kumtaja mtuhumiwa aliyekutwa na silaha hiyo kuwa ni Masanja Machungwa mwenye umri wa miaka 46 mkazi wa  katika kijiji cha Bukundi wilayani Meatu.

Katika hatua nyingine Kamanda Lyanga ameongeza kuwa mbali na tukio hilo la kukutwa nyala za serikali pamoja na silaha polisi mkoani hapa wanamshikilia mtu mmoja aitwaye Musa Noni kwa tuhuma ya kumbaka mtoto mwenye umri miaka 7 ambaye anasoma chekechea katika shule ya msingi Ipililo wilayani Maswa.

Aidha Kamanda Lyanga amewataka wamiliki wa magari na mikokoteni mkoani hapa kuhakikisha wanaweka viakisi mwanga katika vyombo vyao pamoja na kudhibiti mwendo kasi ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kudhibiti ajali mkoani humo.
Credit: ITV

Baada ya Uchaguzi wa Umeya Kuvunjika, Chadema Kwenda Mahakamani Kudai Haki

“CHADEMA ilianzisha Operesheni Umoja wa Kupambana Udikteta Tanzania (UKUTA), hatuwezi kukaa kimya tena, Nyerere alikataza Vijana kuwa wanyonge na waoga, hakutaka Taifa la watu waoga, na sisi tunasema mwisho wa uoga umekwisha, tutakwenda Mahakamani kwa sababu kilichotokea leo kwenye Uchaguzi wa Meya wa Manispaa Kinondoni leo ni uhuni, kanuni na taratibu zinavunjwa waziwazi”

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA Taifa, Dkt. Vincent Mashinji, wakati akiongea na waandishi wa habari Makao Makuu ya Chama hicho yaliyopo Kinondoni jijini Dar es salaam, leo Jumapili 23/10/2016 baada ya Uchaguzi wa kumapata Meya wa Manispaa ya Kinondoni kuvunjika.
Wanatumia vyombo vya dola kudhibiti, Polisi kwenye uchaguzi wamekuwa wengi kuliko wajumbe ili wawatie hofu wajumbe na wananchi waliojitokeza kushuhudia Uchaguzi huo, Polisi wamewazuia kuingia ndani Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wa CHADEMA kushuhudia Uchaguzi huo, vyombo vya habari vinavyoripoti bila kupendelea upande wowote vimezuliwa kuingia, waliozuiwa kuingia ni mwandishi wa Mwananchi, Mtanzania na Tanzania Daima, huku wakiruhusu waandishi wao wa TBC, Uhuru na Mzalendo, unaweza ukaona jinsi nchi inavyoendeshwa na Serikali ya awamu ya tano.

CHADEMA kimesema hakitakuwa Chama cha kulalamika tena, watakwenda Mahakamani, watakusanya ushahidi na kudai haki, Mashinji amesema wameanza kudai Katiba ya Wananchi ndiyo suluhisho ya kila kitu, ni Katiba ambayo ni ya Wananchi ambayo ikipatikana mambo kama haya ya uvunjaji Sheria,kanuni na taratibu katika nchi utakwisha.

Madiwani wa Ukawa walitoka nje ya ukumbi wa kupigia kura mara baada ya kubainika mbinu chafu zilizokuwa zimeandaliwa ili mshindi atoke CCM, Wajumbe kutoka nje ya Manispaa ya Kinondoni wameingizwa kwenye Uchaguzi huo ikiwa ni kinyume na Sheria na taratibu, huku wajumbe halali wa UKAWA wakitolewa kushiriki Uchaguzi huo, waliotolewa ni Mhe. Susan Lyimo na Salma Mwasa.

Akiongea Mhe. Halima Mdee amesema watakwenda Mahakamani kwa kuwa ni ukiukwaji wa sheria, taarifa ya Uchaguzi hutolewa ndani ya siku 7, ili kutafuta wajumbe, kuangalia mkinzano wa kisheria ili mambo yawekwe sawa, lakini kilichofanyika taarifa imetolewa siku 1 kabla ya Uchaguzi ili wafanye mbinu zao ovu, Madiwani wapo 34, ili akidi itimie lazima kura zipigwe 23,lakini wamepiga kura wajumbe 18 tu, huo ni uvunjaji wa Sheria ndo maana CHADEMA imeamua kwenda mahakamani.

EPL: Mourinho aondoka darajani kwa kichapo kikali cha bao 4 - 0

Chelsea Vs Manchester United 4-0: Uwanjani Stamford Bridge kwenye Ligi Kuu England, ambayo ni mechi ya kwanza Jose Mourinho kurejea uwanjani hapo tangu afukuzwe Umeneja Chelsea Desemba 2015.

Man U, wakionyesha kusuasua katika game ya leo, walikuwa nyuma 2-0 hadi mapumziko na Chelsea walipata bao lao la kwanza dakika ya kwanza, sekunde ya 34 tu kupitia Pedro.
Bao la Pili la Chelsea lilifungwa na Gary Cahill.

Kipindi cha pili, Chelsea waliongeza bao nyingine 2 kaika dakika ya 62 na 70 wafungaji wakiwa Hazard na Kante.

Matokeo haya yamewaweka Chelsea nafasi ya 4 wakati Man United wanabaki nafasi ya 7.

Vikosi.
Chelsea:
Courtois; Azpilicueta, David Luiz, Cahill; Moses, Kante, Matic, Alonso; Pedro [Chalobah, 71’], Hazard [Willian, 78’] Diego Costa [Batshuayi, 78’]

Sub: Begovic, Aina, Terry, Chalobah, Oscar, Willian, Batshuayi.

Manchester United:
De Gea; Valencia, Bailly [Rojo, 52’], Smalling, Blind; Herrera, Fellaini [Mata, 45’], Lingard [Martial, 65’], Pogba, Rashford, Ibrahimovic.

Sub: Romero, Rojo, Darmian, Carrick, Young, Mata, Martial.

Refa: Martin Atkinson

Simba Waendeleza Kichapo baada ya kuwacharaza Toto African's Bao 3 - 0 Leo Katika Uwanja wa Uhuru

Mchezo wa simba dhidi ya Toto african's umeisha rasmi katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam, Toto wakilazwa mara tatu dhidi ya wapinzani wao simba.

Simba wamemiliki mpira muda mwingi na kupiga pasi zenye mafaniko ambo ziliwapelekea kuibuka na ushindi mzuri wa goal 3 kwa bila dhidi ya Tota African's ambao walihindwa kabisa kuliona lango la Simba.

Simba walibahatika kupiga kona nyingi ambazo zilikuwa katika haraka za kumchungilia mlinda mlango wa toto. Ata hivyo Toto walikuwa wanajaribu kuwatafuta simba ambapo katika dakika ya 10 Waziri Jr. alipata pasi nzuri na kumchungulia mlinda mlango wa simba lakini ilikuwa tayari Offside, dakika ya 16 walipata faulo nje kidogo ya eneo la 18 la simba baada ya kucheza vzuri,Toto walifanya shambulizi kali katika dakika ya 27 kupia mshambuliaji wao Lusajo lakini akashindwa kumalizia mbele ya lango la Simba.
Simba nao hawakuwa mbali na lango la Toto na hivyo kupelekea mashambulizi mengi zaidi na kona nyingi zaidi lakini katika dakika 43 Simba walipata goli la kwanza kupitia mchezaji wao Mzamiru ambaye aliunganisha kwa uzuri kabisa krosi iliyopigwa na Blagnon na hivyo hadi kipindi cha kwanza kinaisha simba walikuwa wanaongoza kwa bao 1-0.

Baada ya kipindi cha pili kuanza dakika chache Mchezaji wa Simba Blagnon aliumia kichwani baada ya kugongana na beki wa Toto na hivyo kupelekea mpira kusimama kwa dakika kadhaa kabla ya Blagnon kutoka dakika ya 49 na Mavugo kuchukua nafasi yake baada ya kuumia na dakika 3 baada ya kuingia Mavugo anaindikia SIMBA bao la pili baada ya kumalizia vizuri pasi ya Mohammed. Simba walimiliki mpira kwa uzuri kabisa na kufanya mabailiko kadhaa kama kutoka kwa Mwinyi Kazimoto na nafasi yake kuchukuliwa na Jamal Mnyate  na mpira uliendelea wakati lango la Toto likishambuliwa sana na dakika ya 74 Kona iliyopigwa na Kichuya inazaa matunda baada ya kumaliziwa kwa shuti kali kutoka kwa Mzamiru na hivyo kufanya Simba kuwa mbele kwa mabao 3.
Mashambulizi yaliendelea mpaka mwamuzi alipopuliza kipenga kuashiria mpira umekwisha na Simba wakiongoza kwa mabao matatu yaliyafungwa na Mzamiru 2 na Mavugo 1 wakati wapinzani wao (Toto) wakiwa awajapata kuona lango la Simba.

Mechi nyingine zilizochezwa ni
 
Msimamo wa Vodacom Premier league baada ya mechi za leo ni kama ifuatavyo:-
 

Uchaguzi wa Umeya Ubungo Waahirishwa...Kisa chote hiki hapa

Uchaguzi wa kumpata Meya wa Ubungo umeahirishwa leo hadi hapo itakapotangazwa tena baada ya madiwani wa Chadema na CUF kususa wakidai CCM imeongeza wajumbe.

Madiwani hao wamedai wajumbe wawili wa UKAWA wamehamishwa ili kurahisisha ushindi kwa CCM.

Kikosi cha Simba SC Vs Mbao FC Leo

Simba-SC

    Vincent Angban
    Janvier Bokungu
    Mohamed Hussein
    Juuko Murushid
    Method Mwanjali
    Jonas Mkude
    Shiza Kichuya
    Mzamiru Yassin
    Laudit Mavugo
    Ibrahim Migomba
    Mwinyi Kazimoto

Benchi

    Peter Manyika
    Abdi Banda
    Said Juma
    Novaty Lufunga
    Emmanuel Simwanza
    Mohamed Ibrahim
    Gove Blagnon

Rais Barack Obama Asikitishwa na Malalamiko ya Trump

Rais Barack Obama wa Marekani ameyaelezea malalamiko yaliyotolewa na mgombea kupitia chama cha Republican, Donald Trump, kwamba kuna udanganyifu unafanyika katika uchaguzi wa Rais nchini humo, kuwa ni ya hatari na kuharibu demokrasia.

Amemlaumu mgombea huyo wa Republican kutilia shaka uhalali wa uchaguzi huo, bila ya kuwa na ushahidi kamili wa kuwepo kwa hila kwenye uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao.

Wakati wa mdahalo wao wa tatu na wa mwisho uliofanyika jana kati yake na mpinzani wake Hillary Clinton, Bwana Trump alikataa moja kwa moja kusema kwamba atakubali matokeo iwapo atashindwa.
Hata hivyo chama chake cha Republican kimekuwa kikijaribu kusafisha kauli yake hiyo.

Timu ya Kampeni ya uchaguzi ya Bwana Trump inamlaumu Hillary Clinton mgombea kupitia chama cha Democrats kwa kupanga jaribio la kutaka kumchafua mgombea huyo wa Republican baada ya mwanamke wa 10 kujitokeza akiilaumu tabia yake ya kudhalilisha wanawake kijinsia.

Mwana mama huyo Karena Virginia anamtuhumu Bwana Trump kwa kile alichosema alimpapasa kifuani, wakati wa mashindano ya mchezo wa tenisi mwaka 1998.

Kisiwa cha Bongoyo Hatarini Kutoweka

Dar es Salaam. Mabadiliko ya hali ya hewa yanaendelea kukiathiri Kisiwa cha Bongoyo kilichopo jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mhifadhi Mfawidhi wa maeneo tengefu Mkoa wa Dar es Salaam, Jairos Mahenge amesema kuna haja ya kufanya  tafiti ili kupata suluhu kuhusu  nanma ya kukabiliana na mabadiliko hayo.

“Kina cha maji ya Bahari ya Hindi kinazidi kupanda na pepo hazitabiriki…kisiwa kinaonekana kumezwa, hali hii inahatarisha hata utalii wa hapa,” amesema.

Tofauti na kisiwa kilichopo jirani cha Mbudya, Bongoyo hutembelewa idadi kubwa ya wageni kutoka nje ya nchi lakini wahifadhi wanahofia huenda mandhari inayowavutia watalii ikamezwa na bahari.

Kiongozi wa Wahifadhi wa Kujitolea Bongoyo, John Mbuwa amesema ardhi ya kisiwa hicho inaendelea kumomonyoka, jambo lililosababisha kuhamisha banda lao la kuhudumia watalii baada ardhi kumomonyolewa na maji.
Mfaume Majaliwa ambaye ni Mhifadhi wa Kujitolea katika Kisiwa cha Mbudya amesema uchafu wa mazingira Dar es Salaam unahatarisha mandhari ya visiwa hivyo hasa wakati wa masika.

“Uchafu wote unaletwa na maji ya mvua huingia baharini. Hali hii sio nzuri kabisa na watalii hawapendelei. Programu ya usafi ni muhimu iwapo tunataka watalii waendelee kuja kwenye visiwa hivi,” amesema Majaliwa.

Hata hivyo, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imeanza mkakati wa kuvitangaza visiwa hivyo kwa ajili ya kuwavutia watalii zaidi tofauti na sasa Mlima Kilimanjaro, Visiwa vya Zanzibar na hifadhi za wanyama zilizopo kaskazini mwa nchi hutangazwa zaidi.

Kwa kujibu wa Ofisa Masoko wa TTB, Francis Malugu, mkakati uliopo ni kutangaza utalii wa kitamaduni na kuhamasisha Watanzania kufanya utalii wa ndani.

Serikali: Ujio wa Mfalme wa Morocco ni Muhimu

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania kupitia msemaji wake, Hassan Abass imesema ujio wa Mfalme wa Morocco, Mohamed VI ni muhimu kwa uhusiano wa kidiplomasia na uchumi.

“Serikali ilishaeleza msimamo wake, kuna uhusiano wa aina nyingi, ujio huu ni muhimu kwa uhusiano wa kidemokrasia na uchumi kama hisia zitawatuma kufanya hivyo, wanapaswa kufuata sheria,” amesema Abass.

Wakati mfalme  huyo akitarajiwa kuwasili leo nchini kwa ziara ya kikazi, huenda akapokewa kwa mabango baada ya vijana wanaounda kamati ya mshikamano wa Tanzania na Sahara Magharibi (TASSC) kujipanga kufanya hivyo kushinikiza nchi hiyo kuacha kuitawala kwa mabavu Sahara Magharibi.
Vijana hao wamefikia uamuzi huo kutokana na kile walichodai kusikitishwa kwao na kitendo cha Morocco kuendelea kuitawala kwa mabavu nchi ya Sahara Magharibi na kupuuza wito wa Umoja wa Mataifa (UN) unaoitaka kuipa uhuru nchi hiyo.

Bodaboda Zaongoza kwa Ajali na Vifo vya Barabarani

Usafiri wa bodaboda ambao umeanza miaka ya hivi karibuni sasa unaonekana kuchukua maisha ya watu wengi.

Waendesha pikipiki wakipita katika makutano ya Barabara ya Nyerere na Mandela eneo la Mataa ya Tazara, jijini Dar es Salaam.

Takwimu zinaonyesha kuwa bodaboda huchukua maisha ya Watanzania watatu kati ya 17 kila siku.

Ndani ya miaka mitano  ajali za magari na bodaboda kwa ujumla zimesababisha vifo vya watu 30,783 na kujeruhi wengine 141,740.
Miongoni mwa vifo hivyo, 5,518 vimesababishwa na bodaboda pekee.

Takwimu hizo zilizotolewa jana na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga zinaonyesha kuwa miongoni mwa majeruhi wa ajali hizo zilizotokea kuanzia Januari 2010 hadi Septemba mwaka huu, watu 28,341 walikuwa wa pikipiki hizo za kubeba abiria ambazo pia zilisababisha jumla ya ajali 29,136 ikiwa ni zile zilizoripotiwa polisi.
Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top