Star wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja ameibuka na kusema kuwa ushosti wake na Miss Tanzania 2006/07, Wema Sepetu, uliorudishwa hivi karibuni baada ya kuwekana sawa ni wa kinafiki huku akidai Wema ni kigeugeu.
Akizungumza kwa kujiamini mbele ya paparaziwetu, juzi Jumatano pande wa Mikocheni jijini Dar es Salaam, Kajala alisema: “Wema ni mnafiki kabisa. Upatanisho wetu ni wa uongo. Mimi moyoni nimeondoa kinyongo lakini mwenzangu naona kama bado ana donge moyoni.”
Kajala alisema hayo alipoulizwa na Paparaziwetu, sababu ya kutoonekana kwenye tukio la futari lililofanyika nyumbani kwa mama mzazi wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kassim ambaye ni mkwe wa shosti wake huyo.

Kajala Masanja
Katika tukio hilo, mama Diamond alifanyiwa suprise ya nguvu alipokabidhiwa gari kali aina ya Toyota Lexus Harrier kama zawadi ya bethidei yake, ambayo ilitolewa na meneja wa Diamond, Babu Tale kwa niaba ya mwanamuziki huyo ambaye alikuwa safarini nchini Marekani.
Wema Sepetu
“Tunakubaliana kuwa kitu kimoja lakini mwenzangu anaonekana ana kinyongo. Hebu angalia, anawezaje kuacha kunialika kwenye shughuli muhimu kama ile kama kweli tumepatana? Mbona amealika watu wengi lakini mimi ameniacha? Wema aache unafiki bwana.
“Mbaya zaidi, hivi juzi tu ameweka picha ya msichana mmoja anayekaa China, huyu mdada anaitwa Sabrina, niliwahi kugomabana naye, lakini yeye amemuweka Instagram na kumwandikia maneno kibao ya kumsifia akim-wish happy birthday, hapo si kama ananisimanga? Wema si mkweli,” alisema Kajala.
Akizungumzia ishu hiyo, siku ya tukio Wema alisema: “Ukiniuliza kuhusu Kajala kutokuwepo hapa, kwa kweli utakuwa kama unanichanganya tu maana leo sijashika simu muda mrefu sana.
“Hata ujio wangu hapa nilikurupushwa, ndiyo maana sijakumbuka kumuita Kajala, lakini tuko vizuri na mara ya mwisho tumeongea jana (Jumapili) usiku tu,” alisema Wema.
Post a Comment