Kuna matukio ambayo kama binadamu yasikie kwa wengine tu lakini yasikutokee wewe! Kama hili la mkazi wa Ukong- mzambarauni, Dar, Paulo Ndulu ambapo mkesha wa kuamkia Sikukuu ya Sabasaba, alijikuta katika wakati mgumu pale alipoingia kibaruani kuamua ngumi kati ya mkewe, Anitha Mapunda na Elizabeth Chacha aliyedaiwa kuwa ni hawara yake.
Bw. Paulo Ndulu akijaribu kuamua ugomvi kati ya mkewe, Anitha Mapunda na Elizabeth Chacha (mwenye shati nyekundu) anayedaiwa kuwa ni hawara yake.
Siku ya tukio, majira ya saa nane usiku,maeno ya Ukonga jijini Dar kulitokea timbwili zito sana kwenye nyumba ya Ndulu huku majirani kibao wakiama mtaa kushuhudia tukio hili.
Mwandishi wetu alisogea kwenye sekeseke hilo na kugundua kuwa, ndani ya nyumba ya Ndulu kulikuwa na kasheshe zito la nguo kuchanika kati ya wanawakwe wawili ambapo majirani walisema mmoja ni mke, mwingine hawara, kisa?
Mara majirani nao walishuhudia ugomvi uliokuwa ukiendelea kwa kupiga chabo dirishani.
“Mke aliaga anasafiri, mume akaingiza mwanamke mwingine, sasa kumbe mke hakusafiri kikweli, alimdanganya mumewe baada ya kujua kuna mwanamke atakuja,” alisema jirani mmoja huku akilalamika kwamba, amepika daku linapoa kwa sababu ya kushuhudia filamu hiyo ya bure.
Ilidaiwa kuwa, Anitha alikuwa katika wakati mgumu baada ya mumewe kuwa na tabia ya kumwingiza mwanamke huyo ndani na kumwambia yeye akakae mahali anywe soda au aende kwao mpaka mgeni wake atakapoondoka ndipo arudi.
Siku ya tukio, kwa mujibu wa mashuhuda, Anitha alipobaini ujio wa mgeni huyo (Elizabeth) alijifanya anakwenda Kimanzichana, Kisarawe, Pwani lakini uhalisia alikwenda kujificha nyumba ya jirani huku akiweka wapambe wampigie chabo nyendo za mumewe kwa usiku huo kwa sababu alikuwa amechoshwa na uonevu wa kutakiwa kwenda kukaa mahali.
Chanzo kilisema saa moja usiku, Ndulu alionekana akirudi nyumbani hapo. Muda si mrefu, mrembo mweupe, mrefu alionekana akiingia nyumbani hapo na Ndulu alitoka kumpokea.
Jirani huyo alizidi kusema kuwa, wakati Eliza akizama ndani Ndulu, alivua viatu na kuviacha nje ya mlango. Wapambe wakavichukua na kwenda kumuonesha Anitha akiwa mafichoni ili kumthibitishia kuwa tayari mumewe alikuwa na kifaa ndani.
Hawara huyo(Elizabeth Chacha) akikalishwa chini ili wayamalize kiutu uzima.
Baada ya kuoneshwa viatu hivyo, Anitha alichanganyikiwa na kutoka kwenda nyumbani kwake ambapo aliingia na kusababisha varangati hilo la aina yake lililodumu kwa karibu dakika ishirini mpaka mwandishi wetu alipotokea eneo la tukio na pia askari wa kulida doria usiku walitinga eneo la tukio.
Ili kuweka sawa mambo ya kisheria, maafande hao wenye maadili ya kazi walikwenda hadi kwa Mjumbe wa Shina Namba 29, Mama Urio ambaye waliongozana naye mpaka kwenye eneo lenye kizaazaa.Hata hivyo, polisi na mjume huyo walimkuta Anitha ameshamvaa mbaya wake huyo huku akimtupia maneno yenye lawama na shutuma nzitonzito kwamba anamvunjia nyumba yake.
Majirani walifika eneo la tukio na kushudia mkasa huo.
Ndulu mbali ya kuchoka hoi kufuatia kazi nzito na kumdhibiti mkewe asiendelee kuzichapa na Eliza, pia alikuwa na kazi nyingine ya kugombana na majirani ‘wambeya’ walijaa dirishani kwa nje wakimporomoshea maneno yenye kuudhi.
Baada ya hali ya hewa kutulia, polisi walimuhoji Ndulu kuhusu sakata hilo, alikiri kuishi na Anitha kwa zaidi ya miaka minne lakini alimkana kuwa si mkewe kwa kuwa yeye ni Mkristo wa madhehebu ya Katoliki na hakuwahi kufunga naye ndoa.
Hata hivyo, utetezi huo wa Ndulu ulipingwa vikali na mjumbe wa nyumba kumi na polisi ambapo walimwambia kisheria mwanaume na mwanamke wakiishi ndani ya nyumba kwa muda huo tayari ni mkewe.
Wakasema kwa hiyo kitendo cha kumpelekea mwanamke mwingine ndani ni kutafuta machafuko kwa makusudi.
Bw. Paulo Ndulu akijitetea kuhusu uhusiano wake na hawara huyo.
Wakati wote wa sakata, Elizabeth alikuwa akipiga mayowe ya kuomba msaada akisema amekoma kwani Ndulu alimwambia kuwa haishi na mwanamke baada ya kuachana na Anitha muda mrefu kwa sababu za ugumba.
Bi. Elizabeth Chacha akiondoka peku peku eneo la tukio.
"Mimi aliniambia haishi na mwanamke na nilimuuliza sana kuhusu hili naye akanithibitishia kuwa ni msela lakini hata hivyo machale yalikuwa yakinicheza muda wote, namuomba radhi mwanamke mwenzangu jamani,” alisema Eliza.
Hatima ya sakata hilo, Elizabeth alitakiwa kurudi kwao, Ubungo -Maziwa jijini Dar na Anitha alishauriwa kwenda kulala kwa kaka yake anayeishi jirani na eneo hilo chini ya usimamizi wa mjumbe.
Akizungumza na Mwandishi wetu baada ya kutulia kwa sekeseke, Anitha alisema miaka minne ya maisna na Ndulu, mapenzi yalikuwa motomoto lakini siku za karibuni mwanaume huyo alibadilika ghafla, akaamini ni baada ya kumpata Eliza.
Akizungumza na Mwandishi wetu baada ya kutulia kwa sekeseke, Anitha alisema miaka minne ya maisna na Ndulu, mapenzi yalikuwa motomoto lakini siku za karibuni mwanaume huyo alibadilika ghafla, akaamini ni baada ya kumpata Eliza.
Post a Comment