Kesi ya mwanariadha wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius itaendelea Oktoba 21, 2014 mawakili wake wakitaka apewe adhabu ndogo.
Mahakama inayosikiliza kesi dhidi ya mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius imeambiwa kuwa mwanariadha huyo amefilisika.
Pistorius alipatikana na hatia ya mauji ya mpenzi wake Reeva Steenkamp bila ya kukusudia mwaka jana.
Jaji Thokozile Masipa anatarajiwa kutoa hukumu dhidi ya Pistorius Jumanne. Anakabiliwa na kifungo cha miaka 15 lakini jaji anaweza kuamua kumpa kifungo cha nje au hata kumtoza faini. Upande wa mashitaka unataka Pistorius apewe adhabu kubwa kuambatana na kosa lake.
Pistorius aliangua kilio wakili wake alipoambia mahakama kuwa amefilisika Pistorius aliangua kilio wakili wake aliposema kuwa pesa zake zimekwisha baada ya kesi yake kufanya kwa miezi saba. "sio tu kwamba hana pesa bali anahisi hana tena matumaini,'' alisema wakili wa Pistorius.
Mwanariadha wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius akiwa mahakamani siku ya leo. Aimee Pistorius (katikati) akimuangalia kaka yake, Oscar Pistorius wakati wakili wake Barry Roux's akiendelea kumtetea (hayupo pichani), Kulia wa pili ni shangazi yake, Lois akiwa na mjomba wake Arnold (kulia).
Oscar Pistorius akilia baada ya wakili wake kusema kuwa pesa zake zimekwisha baada ya kesi yake kuendeshwa kwa miezi saba.
Kaka yake Oscar Pistorius, Carl Pistorius akifuatilia kesi ya mdogo wake.
Dada yake Oscar Pistorius, Aimee akimsalimia mmoja wa mawakili anayemtetea kaka yake, Brian Webber.
Mama yake marehemu, Reeva Steenkamp's akiwasili mahakamani siku ya leo.
Post a Comment