Mfanyabiashara maarufu mkoani Kilimanjaro, Thadey Salekio (82), amefariki dunia kwa kunaswa na umeme wakati akijaribu kujiunganishia nishati hiyo kienyeji.
Ndugu wa marehemu wamesema kuwa mfanyabiashara huyo alifikwa na umauti baada ya waya aliojaribu kujiunganishia umeme kutoka nguzo jirani kuanguka na kusababisha shock.

Mtoto wa marehemu, Venance Mushi, alisema majira ya alfajiri, baba yake alikutwa amefariki dunia baada ya kupigwa na shoti ya umeme.
“Baba alikuwa anajiandaa kwenda kanisani na gafla alikutana na waya ambao hakujua ni wa nini na alipojaribu kuusogeza ndipo alipopigwa shoti na kutokana na baba huyo kuishi na mjukuu mdogo hakuweza kumsaidia hadi majirani walipofika na inadaiwa tayari alikuwa amesha poteza maisha,” alisema.
Mwenyekiti wa kijiji hicho alisema matukio kama hayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara.
Diwani wa kata ya Kibosho kati, David Mboro, alisema matatizo hayo ya kujiunganishia umeme yamekuwa mengi sana katika Wilaya ya Moshi vijijini hasa maeneo ya tarafa ya Kibosho, ambapo familia zimekuwa zikiteketea na kusababisha ongezeko la watoto wa mitaani mkoani hapa.
Kaimu Meneja wa Shirika la Umeme (Tanesco) mkoa wa Kilimanjaro, Mathius Msolongo, alikiri kuwepo kwa matukio kama hayo mkoani hapa na kusema kuwa wamejipanga katika kutoa elimu juu ya madhara ya kujiunganishia umeme kinyume na sheria.

Post a Comment