MICHEPUKO....Mke,Mume wavuana nguo Hadharani

Njemba mmoja aliyefahamika kwa jina la Zeno na mkewe Mwajuma Mtata, wakazi wa mtaa Mrefu, Kigogo-Luhanga jijini Dar wamenaswa wakiangusha bonge la timbwili barabarani na kusababisha umati wa watu kujikusanya eneo hilo kujionea ‘sinema’ ya bure.Tukio hilo lililofananishwa na muvi ya kivita lilitokea usiku wa Jumanne iliyopita ambapo chanzo kimedaiwa kuwa ni mwanamke huyo kutelekeza jikoni kitoweo cha maini ya mbuzi na kwenda baa kupata kilaji.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, siku ya tukio, Zeno alirudi nyumbani mida ya jioni mkononi akiwa na kifurushi chenye maini ya mbuzi pamoja na mazagazaga mengine zikiwemo ndimu, tangawizi, pilipili hoho, nyanya na vitunguu kupokelewa na mke wake huyo.

Baada ya Zeno kumkabidhi mkewe mazagazaga hayo kwa ajili ya mlo wa usiku, alimuaga mkewe kuwa anakwenda kutembea ili akirudi akute msosi uko tayari, wale, walale.
“Dakika kadhaa baada ya mumewe kutoka, nasikia bibie naye alichomoka na kwenda baa ya jirani ‘kusukutua mdomo’.
 “Sasa akiwa pale baa, alizidi kunogewa na masaa yalizidi kupotea ndipo Zeno alirudi nyumbani na kukuta mlango umeegeshwa na mkewe hayupo huku akisikia harufu kali ya kitu kuungua na kumfanya apige chafya.
“Alipokaa sawa alibaini kuwa maini aliyoleta yalikuwa yameungua na kuwa kama mkaa hali iliyompandisha hasira na kuanza kumsaka mkewe,” kilidai chanzo chetu.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga mavituzi kwamba, Zeno akiwa katika sakasaka yake ndipo alipombamba mkewe kwenye baa hiyo akimalizia ‘kunyonya’ kilevi kikali.
 
Bila kuuliza, Zeno alimkunja mkewe na kumtoa nje huku akimpa makofi ndipo Mwajuma akaona kama anaonewa hivyo akamvizia mumewe na kumchota mtama ambapo wote walikwenda chini kutokana na kuwa katika hali ya kuzidiwa na kinywaji.

Timbwili hilo liliendelea nje ya baa hiyo ambapo vijana wawili wa mtaani hapo waliofahamika kwa majina ya Haidani na Kulwa walihofia yangeweza kutokea machafuko zaidi wakakimbilia kwa mjumbe wa eneo hilo aliyefahamika kwa jina la Shukuru lakini walimkuta mke wa mjumbe ambaye aliwaambia mumewe alikuwa kazini.
Wapenzi hao baada ya kugaragazana vya kutosha ikiwa ni pamoja na kuvuana nguo, mwanaume alianza kumburuza mkewe na kurudi nyumbani kwao ambapo walipofika eneo la Kwamkoma walianza kutifuana tena kabla ya kuamuliwa na wasamaria wema.
Taarifa tulizozipata wakati hadi sasa, wawili hao wameshasameheana, wameshayamaliza na wanaishi raha mustarehe baada ya kuombana msamaha.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top