Mtandao huu umewashuhudia wakazi wa Kunduchi jijini Dar es Salaam, wakiandamana kuelekea vituo vya Polisi vya Wazo na Mtongani, baada ya kudai kuwa ndugu zao wamekamatwa wakiwa hawana makosa na kupelekwa kituoni.
Wakizungumza na mwandishi wetu baadhi ya waandamanaji walisema difenda tano za Polisi zilikwenda eneo hilo na kuanza kukamata watu ovyo kwa madai kuwa ni wahuni na wavuta bangi.
Dereva mmoja wa bodaboda alisema kawaida ya Polisi hao hufika na kuwakamata wahuni, wavuta bangi na vijana walio katika makundi ya uhalifu, ila kilichotokea ni wahuni hao kushtuka na kukimbia, ndipo polisi wakaaanza kukamata watu hovyo hata wasiohusika.
Post a Comment