Ni vema kutambua mambo muhimu ya kuomba ruhusa kwa mpenzi wako kabla ya kukurupuka..

1.Kuchati kwenye mtandao mara baada ya kurudi nyumbani au kama una kazi za ofisini ambazo inakulazimu uzifanyie nyumbani. Ni vyema kumuomba mwenzi wako ruhusa kama hatajali kabla ya kukurupuka na kufungua lap top na kuendelea na kazi zako.
Ni muhimu kuomba ruhusa kwa mwenzi wako kwa sababu huwezi kujua labda kuna jambo alikuwa anataka mjadili au anahitaji muda wa kuwa na wewe.
2.Kama utakuwa na mtoko na wafanyakazi wenzako au marafiki zako. Kwa mfano ile mitoko ya leo tupo club, ni vyema kumjulisha mwenzi wako mapema, ili ajue uko wapi na sio mwenzi wako aje kujua baadae, sababu italeta ugomvi

3.Kama utachelewa kurudi nyumbani kutokana na jambo lolote ni vyema kumjulisha mwenzako, lakini pia hata kama utakula chakula huko ulipo ni vyema pia kumjulisha mwenzako kwa sababu anaweza akawa amekuandalia chakula kizuri halafu usile kitanuka mbaya. kumbuka, miongoni mwa mambo ambayo yanawakera wanawake ni mwanaume kutokula chakula nyumbani ugomvi wake ni MAJANGA....!

4.Kutoa msaada sio kwa vituo vya watoto yatima tu, bali hata kwa ndugu zako, kitu chochote iwe ni nguo au chakula ni au vitu vingine ni vyema kumjulisha mwenzi wako kuliko kufanya mambo kimya kimya. Mwenzako atakapojua anaweza kulalamika au akakaa kimya lakini usije ukadhani ni mjinga kuna siku atalipiza kitu ambacho hutafurahiya.

5.Kuwaeleza mashoga zako kuhusu mipango yenu. Katu usije ukawaambia mashoga zako kwamba mna mpango wa kununua nyumba au kununua gari. Ni vyema mipango yenu ikawa ni siri yenu kwani ikitokea mipango hiyo ikakwama utaishia kuzodolewa na mashoga zako. kumbuka kwamba si kila shoga anapenda maendeleo ya mwingine

6.Ghafla unabadili mtindo wa nywele bila kumshauri mwenza wako. Unaweza kuibua kisirani cha bure katika ushusiano wenu.

7.Kutupa vitu ambavyo unaviona kama uchafu ndani ya nyumba wakti mwenzako alikuwa bado anavihitaji kwa matumizi mengine. Kuna baadhi ya wanawake wanapoamua kusafisha nyumba hutaka kutupa kila kitu anachoona kama ni uchafu bila kumshirikisha mwenzi wake. Ni kosa kubwa, ni vyema kushauriana wakati wa kusafisha nyumba ili kujua ni kitu gani cha kutupa na kitu gani cha kuhifadhi.

8.Kuacha vitu kwa mwenzi wako bila taarifa. Kama mpo katika mahusiano lakini kila mmoja anaishi kwake, pale unapokwenda kupitisha usiku kwa mwenzako ni vyema ukamuuliza kama unataka kuacha baadhi ya vitu vyako hapo kwake kuliko kukurupuka na kuhamishia wardrobe nyumbani kwa mwenzi wako bila taarifa. Utaonekana kama unalazimisha jambo fulani........

9.Kuombaomba. Kuna baadhi ya wanawake au hata wanaume wanapenda kuombaomba misaada kwa wenzi wao. Kuna wengine wako smart wao hutumia neno, "Niazime" lakini si kwamba wanaazima bali wanaomba na hawawezi kurudisha, ni vyema kuwa wastaarabu na kuweka mipaka, hata kama mtu anataka msaada aonyeshe juhudi zake kwanza ndipo labda uombe msaada na sio kila siku anaomba tu mpaka mtu anakuchoka..........

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top