Katika ajali hii ambayo imeua watu 11 na kujeruhi wengine ambayo idadi yao haikufahamika kwa haraka, ilitokea leo asubuhi katika eneo la kona kali ya Mkanyageni mkoani Tanga ikihusisha gari ya abiria aina ya Costa iliyogongana uso kwa uso na Scania Semitrela.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hili wanasema katika ajali hiyo Costa imekatika kati kwa kati na watu waliojeruhiwa wapo kwenye costa hiyo ambayo inafanya safari zake toka mjini Tanga kuelekea Lushoto na Scania iliyokuwa ikitokea Mkanyageni.
Chanzo cha ajali hiyo kimesemekana kuwa ni mwendo kasi wa Dereva.
Post a Comment