Duuh! Picha za Ommy Dimpoz na Wema Sepetu wakiwa kimahaba zazua gumzo mtandaoni....

Zile picha za mahaba zilizosambaa kwenye mitandao zikimuonyesha Staa wa Bongo Fleva,Ommy Dimpoz na Wema Sepetu wakiwa kitandani zimezidi kuzua utata baada ya Ommy kusema hakujua alipigwa saa ngapi kwani hakuwa na fahamu bali aulizwe Wema.
Ommy akizungumza katika  kipindi  cha  Uheard na Soudy Brown amesema kuwa hana maelezo zaidi ya kuzungumza zaidi ya kusema kuwa hajui ni muda upi zilipigwa picha hizo.

Wiki hii picha hizo zilisambaa mitandaoni na kuzua maswali kuwa Ommy Dimpoz ameamua kujiweka kwa Wema baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Diamond Platinum.

Hata  hivyo, Aunty Ezekiel ambaye ni rafiki wa Wema amesema kuwa rafiki yake huyo alikwenda nchini Afrika Kusini kufanya video mpya ya ngoma ya Ommy.

Wiki  hii pia  picha nyingine zilisambaa Wema akiwa na aliyekuwa mume wa Zari wakiponda raha nchini humo na kuzua sintofahamu.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top