Tetesi...Alikiba na Jokate ndani ya penzi zito....................................................................

Kuna tetesi zinavuna kuwa Jokate Mwegelo na Alikiba ni wapenzi!

Tetesi hizo zimekuwepo kwa muda sasa japo wawili hao bado hawajaweza kuthibitisha muungano wao.

Mtangazaji namba moja kwa udaku nchini, Soudy Brown wa Clouds FM alijaribu kumtafuta Jokate kutaka kutegua kitendawili hicho lakini kama ilivyotarajiwa, Jokate aliishia kuangua kicheko tu na kutotoa jibu.
Wafuatiliaji wa mambo wameenda mbali zaidi na kudai kuwa wawili hao wamekuwa wakionekana pamoja kwenye sehemu kadhaa ikiwemo nyumbani kwa Alikiba.

Wengine wamefuatilia baadhi ya picha zao mitandao ya kijamii na kugundua kuwa Jokate amewahi kuivaa kofia ya mkeka ya Alikiba!

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top