Mwigizaji maarufu kutoka nchini Kenya Mzee Ojwang amefaiki dunia jana jumapili jioni katika hospitali ya Kenyatta jijini Nairobi alikokuwa amelazwa, Mwigizaji Benson Wanjau, Mzee Ojwang. Mzee Ojwang alikuwa amelazwa hospitalini hapo akisumbuliwa na ugonjwa wa Pneumonia. Mzee Ojwang alikuwa mwigizaji wa vipindi maarufu vya Vitimbi, Vioja Mahakami, Vituko na Kinyonga katika vituo vya luninga za Kenya na ITV Tanzania.
Mzee Ojwang alijipatia umaarufu nchini Kenya pamoja na maeneo yote ya nchi za Afrika Mashariki kutokana na uwezo wake katika kuigiza ambapo alikuwa akiwavunja mbavu watazamaji wake kutokana na vituko vyake na uwezo wake katika kuchekesha watazamaji wakati akiigiza, Mungu iweke mahali pema peponi roho ya Mwigizaji Marehemu Benson Wanjau alias Mzee Ojwang kwa.
Post a Comment