Udaku: Quick Racka na Kajala katika mahaba mazito...



Rapa mwenye style nyingi na anayejulikana kwa jina maarufu la Quick Rocka amefafanua kwa uwazi fununu zinazozagaa mtaani kwamba yeye na msanii wa bongo movie Kajala Masanja ni wapenzi.
Akiongea na mwandishi wetu mapema leo asubuhi Quick Rocka amepinga uvumi huo na kusema kwamba yeye na Kajala ni marafiki tu wakawaida.
“Kajala sio mpenzi wangu, but she is my best friend na tunafanya kazi kwa karibu”, alisema Quick baada ya kutakiwa kufafanua kuhusu uhusiano wake wa karibu na Kajala.
Quick pia alifunguka kuhusu studio yake ya The Switch ambayo ipo maeneo ya Sinza – Kivulini jijini Dar Es Salaam na kusema kwamba sasa hivi amepata Producer mwingine anayeitwa Lufa baada ya aliyekuwa Producer wa kwanza Nahreel kupata studio nyingine ya kufanyia kazi.
“Tunashukuru Mungu studio inaendelea poa, mpaka sasa tunafahamika, tumetoa wimbo wa Bilima wa msanii Nuhu Mziwanda na hivi karibuni nyimbo za mwasiti na Madee za sikika pia zikitoka Switcher Studio”, alieleza Quick Rocka.
Quick Rocka alimalizia kwa kuweka wazi ukweli juu ya kundi lao la The Rocka na kusema kwamba ni ngumu kundi kurudi hivi karibuni sababu kila member ana mishe zake.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top