Watu 2 wauawa kwa kupigwa na kuchomwa moto kwa tuhuma za wizi mkoani Singida



Watu wawili wenye jinsia ya kiume ambao hawakujulikana mara moja wanaosadikiwa kuwa ni wezi wameuwawa na watu wenye hasira kali kwa kupigwa na kuchomwa moto hadi kufa.

Akielezea tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida ACP.Thobias Sedoyeka pamoja na kuwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi,watu hao ambao inadaiwa kuwa ni wezi ambao wamekuwa wikiiba maeneo hayo mara kwa mara na ndipo wananchi walipoa amua kuchukuwa sheria mkonini ya kuwauwa.

Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Singida Dk.Ramadhani Kabala amethibitisha kupokea maiti mbili ambazo zimeungua vibaya na kuwataka wananchi au nduzao kufika katika hospitali ya mkoa wa Singida kwa ajili ya kuweza kuwatambua.

Kwa upande wao wananchi na mashuhuda wa tukio hilo wametupia lawama kwa baadhi ya vijana wengi siku hizi hawataki kujishugulisha na kujijipatia kipato kwa halali na kupenda kupata fedha za haraka,pia wezi hao siku moja kabla hawaja kutwa na mauti ina semekana nyumba moja ililibiwa,jambo ambalo lilisababisha vijana  kufanya doria  ya sungusungu ili kuweza kuwabaini wezi hao.

Katika hatua nyingine kamanda Sedoyeka amepiga marufuku  mikusanyiko isiyo ya lazima pamoja na disco toto kwenye kumbi zote za starehe katika kipindi cha sikuku ya idi elfitri na kwamba jeshi hilo limejipanga kuhakikisha ulinzi na usalama una imarishwa.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top