Hizi ndizo Tshirt zinazogombaniwa na wananchi Jangwani, Lowassa kiongozi wa Malo...

Nimepita hapa Jangwani kwenye uzinduzi wa kampeni za UKAWA, mchana huu saa 8:45, kitu nilichokishuhudia, Kama Kipimo Cha Ushindi ni Idadi ya Watu, then, Lowassa Ndiye Rais Wetu!. Kwa upande huu wa idadi ya watu wa leo, nikilinganisha na idadi ya watu siku ya ufunguzi wa Mkutano wa CCM, then, CCM imepigwa chini, imeangushwa Chali!, Imeshindwa Vibaya!.

Hii inamaanisha, kama umati huu wote wamejiandikisha, na wote watajitokeza kupiga kura hiyo siku ya uchaguzi, hata CCM waibe vipi kura, kwa kuitumia NEC, kura hazitatosha, mshindi wa uchaguzi huu bado atakuwa ni Edward Lowassa!.


Lakini kama ni kweli, hawa wenye boda boda, bajaj na umati uliojitokeza wamehongwa pesa ili kuleta tuu ujazo wa wingi wa watu, lakini hawajajiandikisha kupiga kura na sii wapiga kura, then hakuna ubishi, mshindi ataendelea kuwa ni CCM!.

Pasco wa jf, sio mwanachama, mfuasi au mshabiki wa chama chochote cha siasa, au mgombea yoyote, bali ni mkereketwa wa demokrasia ya kweli ndani ya bunge, ambaye anaamini kwenye ukweli na uwazi!.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top