Kampeni za ukawa zafunguliwa rasmi leo jangwani bila uwepo wa Dr. SLAA

MRATIBU wa Maandalizi ya Kampeni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Deogratia Munishi amesema maandalizi ya mkutano wa ufunguzi wa kampeni yamekamilika kwa asilimia 90.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika viwanja hivyo vya Jangwani, Munishi amesema kila kitu kipo tayari katika maandalizi hayo na wanachosubiri ni mkutano.
Munishi amesema mkutano huo wa ufunguzi wa kampeni umepangwa kuanza saa 4 asubuhi na kumalizika saa 12 jioni.
Amesema, mkutano utahudhuliwa na watu kutoka sehemu mbalimbali nchini wakiwemo wanachama kutoka nje ya nchi kama Zambia na sehemu nyingine duniani.

Aidha, amewataja viongozi watakaohutubia katika mkutano huo kuwa, Mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa, Mgombea Mweza, Juma Duni Haji, viongozi wakuu wa UKAWA na wawakilishi kutoka makundi mbalimbali.
Kuhusu uwepo wa wasanii katika mkutano huo amesema: “Wasanii watakuwepo lakini hawatapamba mkutano kama kule kwa wenzetu, sisi tunakuja kutangaza sera na sio tamasha la wasanii.”
Naye Afisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene ametoa ratiba ya Mgombea urais na mgombea mwenza kuwa, mara baada ya uzinduzi wa kampeni hizo wataanza ziara mikoani.
Amesema Lowassa, Jumapili ataanza ziara yake Mkoani Iringa na kufanya mikutano ya hadhara minne ambapo ataanzia Mufindi, Kilolo, Karenga, na Iringa Mjini kila sehemu mkutano mmoja.

Kwa Upande wa Babu Duni, amesema ataanzia Mtwara katika wilaya ya Newala, Tandahimba, Mtwara vijijini na Mtwara mjini.
Aidha, kuhusu tetesi za uwepo wa Katibu mkuu Chadema, Dk. Willbrod Slaa viwanja vya jangwani Makene amesema: “Hizo ni tetesi tu. Hakuna ukweli wowote. Dk. Slaa (Willbrod) amepumzika acheni kumzushia maneno.”
Ameongeza, mkutano utakuwa laivu katika televisheni na radio zisizopungua tano kuanzia saa 9 hadi 12 jioni.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top