Kamera ya
mtandao huu imelimulika tukio baya la ajari iliyohusisha pikipiki mbili
eneo la Club Royal karibu na lango la kuingilia chuo cha Utumishi wa
Umma cha Tabora zamani UHAZILI.
Mfuatiliaji
wa tukio alibainisha dereva mmoja alikuwa anatokwa na harufu ya pombe
kitu kilichodhihirisha kuwa alikuwa amelewa huku kamchukua abiria na
akiendesha chombo cha moto.
Mashuhuda
waliuambia mtandao huu kuwa wanalalamikia jeshi la polisi kuto
kujitokeza mapema eneo la tukio licha ya kuwa hapana umbali unaozidi
mita 100 kutoka eneo la tukio, mfuatiliaji wa tukio aliwahoji kama kuna
yeyote aliyetoa taarifa kituoni dhidi ya tukio hilo lakini hakupata
majibu.
Kasendeka
akiwa anazinduka ziduka, akili inakuja baada ya kuzimia kwa muda kidogo
kufuatia ajali iliyohusisha pikipiki mbili eneo la Club Royal karibu na
lango/ geti la kuingilia Chuo Cha Utumishi wa Umma zamani UHAZILI.
Abiria na
mhanga wa ajali hiyo akiwa anaugulia maumivu baada ya ajali iliyotokea
muda mfupi maeneo ya Club Royal karibu na geti kuu la kuingilia Chuo Cha
Utumishi wa Umma zamani UHAZILI
Mashuhuda wa tukio la ajali iliyohusisha pikipiki mbili maeneo ya Club Royal
Kasendeka akiwa anaangalia pikipiki yake baada ya ajali hiyo muda mfupi alipozinduka.
Askari wa
Jeshi la usalama barabarani akijongea eneo la tukio. Inakadiriwa ni
zaidi ya dakika 15 au zaidi (Kwa mujibu wa mashuhuda) zilipita ndipo
askari alijitokeza eneo la tukio licha ya tukio hilo kutokea umbali wa
mita za makadirio zisizozidi 100 kutoka kituo kukuu cha Polisi mjini
Tabora.
Askari akifuatilia tukio hilo baada ya dakika zinazokadiriwa na mashuhuda wa tukio kuwa ni zaidi ya 15 toka ajari imetokea.
Askari
akimhoji Kasendeka kabla ya kwenda naye kituoni huku mhanga mmojawapo
kuwa tayari alishakimbia eneo la tukio na kuisaliti pikipiki eneo la
tukio.
Post a Comment