Mgombea urais wa vyama vinavyounda UKAWA Mh Edward Lowassa ameendelea na ziara ya kunadi sera zilizoko kwenye ilani ya UKAWA katika mkoa wa Ruvuma na kupata mapokezi makubwa na amesema akifanikiwa kuwa rais atayapatia ufumbuzi matatizo sugu yanayowakera wananchi kwa muda mfupi na kuhakikisha maisha yao yanabadilika.
Mh Lowassa aliyeambatana na viongozi wengine wa UKAWA wakiwa katika mji wa Songea ambao walipokelewa na maelfu ya wananchi amesema viongozi wa UKAWA wamejipanga kuwatumikia watanzania kwa vitendo na wala sio kwa maneno na ahadi zisizotekelezeka.

Awali akiwa katika jimbo la Madaba Mh Lowassa aliwaomba wananchi kuona umuhimu wa kupokea mabadiliko.
Kwa upande wao viongozi wengine wa chama hicho waliambatana na Mh Lowassa wameendelea kuwataka wananchi kupuuza maneno yanayosemwa na watu wasiopenda mabadiliko ambayo asilimia kubwa yanalenga kuwakatisha tamaa.
Baadhi ya wananchi na viongozi wakiwemo wa wilaya za mkoa wa Ruvuma wamesema utaratibu wa ahadi zisizo na vitendo umechangia kuongeza makali ya maisha ya wananchi hasa vijijini na kwamba njia pekee ya kuondokana na tatizo hilo ni kukubali mabadiliko kwani sasa wamechoka.
Post a Comment