Wakazi wa Masasi wakiwa wamefurika kwenye uwanja wa Bomani wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia mjini humo,Magufuli aliwaambia wananchi hao kuwa kama atapewa ridhaa na wananchi hao ya kuiongoza Tanzania basi atahakikisha utendaji, ufanisi katika kuleta maendeleo nchini unaongezeka ikiwa pamoja na kuhakikisha kila mwananchi anapata haki ya msingi.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Masasi kwenye uwanja wa Bomani ambapo aliwaambia kama atapewa ridhaa na wananchi hao ya kuiongoza Tanzania basi atahakikisha utendaji, ufanisi katika kuleta maendeleo nchini unaongezeka ikiwa pamoja na kuhakikisha kila mwananchi anapata haki ya msingi.
Mgombea wa Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe akimsikiliza Mwenyekiti wa CCM mkoani Mtwara Ndugu Mohamed Sinan wakati alipokuwa akimkaribisha ili kuzungumza na wakazi wa Nanyumbu mkoani Mtwara.
Wananchi wa Nanyumbu wilayani Masasi wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia mapema leo wilayani humo.
Wananchi wa Nanyumba wakimshangilia Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili na kuwahutubia
Umati wa watu ndani ya uwanja wa Bomani wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia ndani ya mji huo.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwatambulisha wagombea udiwani wa Jimbo la Namtumbo.
Wananchi wa Tunduru wakifurahia jambo kwenye mkutano wa Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Post a Comment