Katika hali isiyo ya kawaida,Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dr. John Magufuli jana alijikuta katika wakati mgumu baada ya kukutana na zomea zomea ya kundi la vijana waliovamia msafara wake akiwa njianI kuelekea Mbarali na kuanza kuimba wakidai Lowassa ndo Rais wao....
Magufuli aliyewasili katika Uwanja wa Ndege wa Songwe, mkoani Mbeya saa tatu asubuhi na kuanza safari ya kwenda Mbarali, alikabiliwa na zomea zomea hiyo katika eneo la Soweto na Uyole.
Wafuasi hao wa Chadema waliuzuia msafara wa Magufuli huku wakionyesha alama ya vidole viwili juu, huku wengine wakizungusha mikono kama ishara ya mabadiliko inayotumiwa na chama hicho na kuimba Lowassa! Lowassa! Lowassa!
Baada ya kuona hivyo, Dk Magufuli aliwaomba wana-Chadema hao wamchague ili afanye mabadiliko bila kujali itikadi za vyama vyao.
Alisema akichaguliwa kuwa rais ataufanyia mabadiliko mji wa Mbeya kuwa M4C, “Sasa itakuwa Mbeya for Change kuwa kituo cha mabadiliko”
“Nikiwa rais, nitakuwa rais wa wote, nitakuwa Rais wa CCM, CUF, Chadema na hata wasio na vyama.
“Chadema oyeeeee, people,s....” Dk Magufuli aliwasalimia wananchi hao kwa salamu inayotumiwa na Chadema, nao wakamwitikia kwa sauti ya juu, ‘power’.
Alisema anatambua kuwa Mbeya kuna wafuasi wa Chadema na kuwataka wafuasi hao kumpa kura ili awaletee maendeleo. Alisisitiza kuwa Serikali yake itahakikisha vijana wote wanapata ajira ili waweze kujitegemea.
“Chadema mnasema people’s power, basi mnipe hiyo power ili niwaletee maendeleo,” alisema mgombea huyo na kuendelea na safari yake kwenda Mbarali.
Post a Comment