Dar es Salaam. Rais John Magufuli amefanya uteuzi wa makatibu tawala wa mikoa 25 na kuwabwaga wanane, waliokuwa wanashikilia nafasi hizo.
Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi ilieleza kuwa kati ya makatibu tawala hao, 10 ni wapya wawili wamebadilishiwa vituo vya kazi na 13 wamebakishwa kwenye vituo vyao vya sasa.
Wapya ambao wataapishwa Ikulu kesho asubuhi ni Richard Kwitega (Arusha), Selestina Gesimba (Geita), Armatus Msole (Kagera) na Aisha Amour (Kilimanjaro).
Wengine ni Zuberi Samataba (Pwani), Albert Msovela (Shinyanga), Dk Angelina Lutambi (Singida). Jumanne Sagini anakwenda Simiyu, Dk Thea Ntara (Tabora) ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Zena Said (Tanga).
Makatibu tawala waliobadilishwa vituo ni Charles Pallangyo kutoka Geita kwenda Kigoma na Dk John Ndunguru kutoka Kigoma kwenda Morogoro.
Waliobakishwa vituo vya kazi ni Theresia Mbando (Dar es Salaam), Rehema Madenge (Dodoma), Wamoja Dickolagwa (Iringa) na Paul Chagonja (Katavi).
Wengine ni Ramadhan Kaswa (Lindi), Benedict Ole Kuyan (Mara), Eliakimu Maswi (Manyara), Mariam Amri (Mbeya), Alfred Luanda (Mtwara).
Kamishna Mathew Mtweve (Mwanza), Jackson Saitabau (Njombe), Symthies Pangisa (Rukwa) na Hassan Bendeyeko (Ruvuma).
Post a Comment