Fahamu njia 10 wanawake hutumia kutongoza wanaume bila kujulikana...

Nina uhakika mkubwa wewe kama mwanaume ushawahi kutongozwa na mwanamke bila kujitambua. Na pia nina uhakika mkubwa zaidi wewe kama mwanamke ushawahi kumtongoza mwanaume kwa njia flani ambayo ulitaka usijulikane. So kama wewe ni mwanaume au kama wewe ni mwanamke nimeamua kuumwaga mtama kueleza mbinu zote ambazo hutumiwa na wanawake kutongoza wanaume kwa njia ya kisiri.

Ok. Kabla tuanze kuorodhesha njia hizi 10 ambazo wanawake hutumia kutongoza wanaume, tunafaa kuelewa ya kwamba wanawake wanaamini kuwa mwanaume ni kiumbe ambacho haelewi chochote kuhusu wanawake...hata akitaka kujua kila kitu kuhusu mwanamke kile atakachopata ni asilimia 10% ya yote ambayo mwanamke anayojua so kuweka hii orodha hapa ni baadhi tu ya njia ambazo wanawake hutumia.

Njia zenyewe ndizo hizi (Psss! wanawake jaribuni kutumia hizi mbinu kama kuna mwanaume unayemzia na haonyeshi dalili za mshiko kwako)

1. Kuikunja miguu
Wanawake hutumia mbinu ya kuikunja miguu yao kimtindo ambapo wanajaribu kuonyesha shepu ya mwili aka kiuno. Ukiona mwanamke anapenda sana kuikunja miguu yake pindi unapokuwa umekaa na yeye mnaongea ni moja wapo ya dalili.

2. Kupapasa na kurusha nywele zake
Hii ni mbinu ambayo hutumiwa sana na wanawake lakini mpaka sahizi wanaume wengi hawajafahamu kama hii ni mbinu moja wapo wanawake hutumia kutongoza wanaume. Pia kama unataka kujua kuwa mwanamke anakutongoza angalia vile hairstyle yake anavyoiweka. Ukiona mwanamke kawaida nywele zake anazifanya zilale nyuma lakini mara moja ama nyingine huweka baadhi ya nywele zake karibu na macho kama yuko na wewe basi fahamu hio ni mbinu anayoitumia kukutongoza.

3. Kujipamba kila baada ya dakika tano
Ushawahi kuongea na mwanamke halafu baada ya dakika fulani anaomba ruhusa ya kuenda msalani? Halafu inatokea mara kwa mara tatizo ni hilo hilo la kuenda msalani kila anapokuwa na wewe? Ushajiuliza ni kwanini? Owk acha nikufungue macho. Mwanamke akikuomba ruhusa kuenda msalani huwa mara nyingi anaenda kujipodoa mbele ya kioo. Ukiwa makini utakuwa umegundua kila anapotoka msalani huwa anapendeza zaidi. Well, sijui anajipaka nini akiwa huko msalani lakini hio ni moja ya dalili ya kuonyesha kuwa mwanamke anakutongoza.

4. Kufinya jicho
Wanaume wengine wanaweza kufinyiwa jicho na mwanamke bila wao kufahamu chochote. Ni wachache pekee ndio wanaweza kutambua hilo na kuchukua hatua ya pili. Hii pointi naona inajieleza yenyewe manake kufinyia mtu jicho inaonyesha kuwa umependezwa na kitu fulani na wala si kuwa umeingiwa na uchafu kwa jicho.

5. Kutabasamu na kuchekacheka
Wanawake wanatumia mbinu hii ili kumfanya mwanaume ajione kuwa yeye anaongea vitu ambavyo vinafurahisha. Kama unamjua mwanamke ambaye anapenda sana kucheka chochote unachoongea basi usipoteze nafasi zaidi. Anza kampeni ya kumnasua awe wako na mapema.

6. Kuleta wivu
Wanawake wengi hawapendi kuongea kuhusu mambo ya nyuma waliyoyapitia awali. Lakini ukikutana na mwanamke ambaye anafunguka moyo wake na kuanza kuelezea mambo yake, wapenzi wake wa zamani na jinsi anawachukia baadhi ya waname ujue ni dalili moja ya kukuonyesha kuwa amelike kampany yako. Ikifika hapa fanya fasta kabla hujapoteza.

7. Kupenda kukusifu
Ukiona unafanya jambo halafu baada ya hapo mwanamke anakusifia ujue amependezwa na wewe. Hii inaweza kuwa vile ulivyovalia, mitindo yako ya maisha unayopenda kufanya ama chochote kile ukiona anapenda kukusifia ujue kuwa 'anataka kitu' kutoka kwako.

8. Whatsapp yako ama facebook yako haitoki
Mitandao ya kijamii ni moja wapo ya njia rahisi kwa mtu kujieleza ya moyo wake bila kujishuku hivyo ukiona mwanamke anakuapproach na kutaka stori kwa whatsapp ama facebook yako usimlenge. Chukua hatua ya haraka kuhakikisha kuwa unaongeza uhusiano wake na wako.

9. Kutafuna ubani ama ballgum
Owk hii nilikuwa nikiipinga mpaka nikaja kuuliza baadhi ya wanawake kuhusu utafunaji wa ubani kama ni mbinu moja wapo ya kutongoza na bila kupinga walikubali. Pia si mara ya kwanza kuambiwa na baadhi ya wanaume kuwa wanapenda vile wanawake wanavyotafuna ubani.

Utafunaji wa ubani humpa nafasi mwanamke kuondoa midomo yake vile anavyotaka yeye hivyo imebainisha kuwa ni mbinu moja wapo ambayo huitumia kutongoza.

10.  Kutuma jumbe za usiku mwema
Kama vile ilivyobainika na wanasayansi kuwa meseji inayotumiwa mtu wakati wa mwisho kabla hajalala ndio mtu atakayemfikiria wakati anapoamka. Ni dhahiri kuwa kuna ukweli wake kiasi flani. Hivyo hivyo ukiona kuwa mwanamke anakutumia text wakati wa usiku wa kiza fahamu kuna kitu kiko jikoni.
Kama ungependa kuunga ama kupinga post hii hebu weka maoni yako hapo chini. Unaweza kuongeza maoni yako kuhusu swala hili zima.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top