Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amewasimamisha vigogo wawili wa Shirika la Ndege Tanzania (ATC) kwa tuhuma za kufanya figisufigisu katika masuala ya uteuzi wa marubani wanaotakiwa kwenda kusoma nje ya nchi.
Mbarawa amedokeza hayo leo alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa walio chini ya wizara yake katika Bandari ya Itunge wilayani Kyela ambapo alisisitiza kwamba hawataki wafanyakazi wababaishaji.
“Leo asubuhi nimewasimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu Kapteni Johnson Mfinanga wa ATC na Mkurugenzi wa Kitengo cha Uendeshaji katika shirika hilo, Sadick Muze wa shirika hilo kwa sababu za kufanya kazi kwa ubabaisha’’ amesema.

Post a Comment