Washitakiwa 3 wa familia moja wafikisha mahakamani Kinondoni kwa mauaji ya dada yao.

Washitakiwa watatu wa familia moja, wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Kinondoni kwa kudaiwa kuhusika na mauaji ya dada yao marehemu Selina Stivin Bugaisa kilichotokea hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo la mauajii ya marehemu Selina Stivin Bugaisa (46) ilitokea mnano 26 julai 2016 katika nyumba ya baba yao aliyekuwa kamishna wa madini Tanzania marehemu Stivin Rwechungura Bugaisa ambapo alikuwa akiisha katika nyumba hiyo eneo la boko CCM baada ya kuachiwa urithi wa nyumba yeye marehemu pamoja na dada yake mwingine aitwae Stela ambaye walizaliwa mapacha anayeishi mkoa wa Arusha kwa sasa.

Watoto wengine wa famili hiyo ambao ni wanaume watatu inasemekana kuwa kila mmoja alijengewa nyumba yake wakati wa uhai wa baba yao ambapo nyumba aliyokuwa akiishi baba yao na mama yao ndiyo ilirithishwa kwa watoto wa kike akiwemo marehemu.

Kutokana na mzozozo mzito wa nyumba hiyo kati ya watoto wa wakiume na watoto wa kike, mara nyingi inasemekana marehemu alikuwa akipata vitisho kutoka kwa nduguze wanaume juu ya nyumba hiyo ambapo ilipofika mnamo 26 Julai 2016 saa 4 usiku marehemu aliingiliwa na watu wasiojulikana na kumuua ndani ya nyumba hiyo na kisha kuviringisha mwili wake na shuka na kumficha uvunguni mwa kitanda ambapo baada ya siku kadhaa kifo chake kikajulikana na alizikwa katika makaburi ya kwa Kondo eneo la Bahari Beach jijini Dar es Salaam.

Kutokana na kifo cha marehemu kuvuta hisia za watu, jeshi la polisi walifanikwa kufanya kazi yao ambapo washtakiwa hao ambao ni watoto watatu wa kiume wa famili hiyo ambao ni Robert Bugaisa, Richard Bugaisa na Godfrey Bugaisa wamefikishwa katika mahakama hiyo ambapo kesi hiyo ya mauaji imesomwa mbele ya Mheshimiwa hakimu Anifa Mwingira ambapo washtakiwa hao hawakuruhusiwa kujibu lolote kwani mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza mashauri hayo ya mauaji.

Upande wa mashtaka uliileza mahakama kuwa upelelezi bado unaendelea hivyo shauri hilo imepangwa tena kutajwa tarehe 26 Agost 2016 huku mwendesha mashtaka wakili wa serikali Doroth Masewe amesema washtakiwa wote kwa pamoja wamerejeshwa mahabusu mpaka tarehe hiyo iliyotajwa ili kutoa nafasi ya upelelezi kukamilika.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright RAHA TAMU Published.. Blogger
Back To Top